TIB YAWEKEZA ZAIDI YA SHILINGI BILIONI 630 ZA UTEKELEZAJI WA MIRADI YA MAENDELEO

Na Mwandishi wetu Dodoma

Benki ya Maendeleo (TIB) inajivunia kutekeleza malengo ya Serikali kwa kuwekeza zaidi ya Shilingi 630.3 bilioni katika miradi ya maendeleo ambazo zimezalisha zaidi ya ajira mpya 12,547.

Mkurugenzi Mtendaji wa Benki huyo Lilian Mbassy ameyazungumza hayo katika Mkutano na waandishi wa habari kuhusu mafanikio na mwelekeo wa Benki hiyo katika kipindi cha miaka minne ya Serikali ya Awamu ya Sita leo Machi 20, 2025, katika Ofisi za Idara ya Habari – MAELEZO, jijini Dodoma.

Mbassy amesema kuwa uwekezaji huo umegusa maeneo ya kipaumbele ya Serikali pamoja na Malengo ya Maendeleo Endelevu (SDGs) hasa katika Shilingi 162.7 bilioni zimewekezwa kuongeza usalama wa chakula na kupunguza njaa, Shilingi 4.3 bilioni zimewekezwa kuboresha elimu kupitia miradi ya taasisi za elimu, Shilingi 22.4 bilioni zimewekezwa katika upatikanaji wa maji safi na usafi wa mazingira kupitia miradi ya mamlaka za maji.

Uwekezaji mwengine ni Shilingi 11.5 bilioni zimewekezwa katika nishati safi na nafuu kupitia mradi wa upanuzi wa nishati ya umeme vijijini (Tanzania Rural Electrification Expansion Programme-TREEP), Shilingi 250.7 bilioni zimewekezwa katika ukuaji wa uchumi na ajira, ikihusisha sekta za utalii, viwanda, na usafirishaji na Shilingi 24.7 bilioni zimewekezwa kuboresha miji na makazi.

Akizungumzia mwelekeo wa utekelezaji wa majukumu ya Benki hiyo, Mbassy amesema TIB kama benki ya maendeleo ni taasisi ya kisera ambayo ina jukumu la kuunga mkono juhudi za Serikali katika kutekeleza sera na mikakati ya kitaifa hususani kwenye utekelezaji wa miradi ya maendeleo

“Katika mwaka 2025 Benki vipaumbele vyake vimejikita katika kuunga mkono juhudi za Serikali katika kutekeleza sera na mikakati ya Kitaifa ili kuongeza kasi ya maendeleo, pamoja na kutekeleza vipaumbele vya Serikali ya Awamu ya Sita.

Amesema kuwa Benki itaendelea kukuza mtaji wa Benki kwa kushirikiana na taasisi za fedha za Kimataifa ili kupata mikopo ya riba nafuu kwaajili ya kufadhili miradi mikubwa ya maendeleo yenye athari Chanya kwa jamii na uchumi.

Kupitia mradi wa upanuzi wa nishati ya umeme vijijini (Tanzania Rural Electrification Expansion Programme-TREEP), Benki inaendelea kushirikiana na Benki ya Dunia kupitia

Hata hivyo benki hiyo imeripoti kuwekeza zaidi ya Shilingi bilioni 630.3 katika miradi ya maendeleo hadi kufikia Desemba 2024, Kati ya kiasi hicho, Shilingi bilioni 408.3 zipo kwenye mizania ya Benki, huku mifuko tisa inayosimamiwa na Benki ikichangia uwekezaji

wa Shilingi bilioni 222. Uwekezaji huo ni wamiradi ya muda wa miaka 5-15 katika Sekta mbalimbali za maendeleo.





Related Posts