Katika kuhakikisha miradi yote ya maendeleo inaleta tija kwa wananchi wilayani Ilala, Mkoani Dar es salaam, Mkuu wa wilaya hiyo Edward Mpogolo ameagiza viporo vyote vikamilike.
Mkuu huyo wa wilaya ya Ilala, ametoa wito huo katika siku ya kwanza ya ziara yake ya kukagua miradi ya maendeleo kwenye sekta ya Afya, elimu na miundombinu ya barabara.
Akiwa katika mradi wa kituo cha afya Mvuti, Mpogolo amepokea taarifa ya utekelezaji wa mradi wa kituo kilichojengwa kwa thamani ya shilingi miliini 500 kutoka kwa Mganga Mkuu wa Jiji la Dar es salaam Zaituni Hamza.
Ambaye ameeleza maendeleo ya ujenzi wa kituo cha afya mradi ambao una lengo la kusogeza huduma ya afya karibu na kupunguza msongamano katika vituo na hospital za rufaa pindi utapoanza kutumika.
Miradi mingine aliyokagua Mkuu wa wilaya ya Ilala, Edward Mpogolo na kupokea taarifa ni sekta ya elimu ya sekondary ambapo ameagiza hadi ifikapo april mosi mwaka huu shule hizo zianze kupokea wanafunzi.
Mpogolo ametoa maagizo hayo kwa Mkuu wa Shule ya Sekondari Kigenzi chini na Mkuu wa Sekomdari Yongwe ambazo ujenzi wa shule hizo umevuka asilimia 90.
Kwa upande wa Mkuu wa Shule ya Sekondari Yongwe Carl Chiwangu ameeleza mradi huo ulipokea fedha milioni 350 chini ya miradi ya Kishindo cha Mama.
Fedha ambazo zimetumika kujenga Madarasa 6, ofisi 2 , maabara, na jengo la utawala, pamoja na miumdombinu mingine.
Aidha Mkuu wa wilaya ya Ilala, Edward Mpogolo , amempongeza Mkurugenzi wa Halmashauri ya Jiji la Ilala Elihuruma Mabelya kwa kazi kubwa anayoifanya kuhakikisha miradi yote iliyokwama inakamilika na kuanza kutumika kwa wakati.