Vita ya Ligi Kuu Bara kuhamia Ivory Coast Leo

Kenya, ikiwa na kiu ya pointi ili kurekebisha kampeni yao ya kufuzu kwa Kombe la Dunia la 2026, inakutana na Gambia kwa mara ya kwanza katika historia leo mjini Abidjan, Ivory Coast.

Mechi hiyo ya kufuzu kwa Kundi “F” itachezwa leo kuanzia saa 10 jioni kwenye Uwanja wa Stade Alassane Ouattara wenye uwezo wa kubeba mashabiki 60,000, ambao ulitumiwa kwa fainali ya Kombe la Mataifa ya Afrika mwaka 2023.

Gambia inacheza mechi hii nyumbani huko Ivory Coast kwa sababu hakuna uwanja uliokidhi vigezo vya FIFA nchini mwao.

Timu ya taifa ya Kenya (Harambee Stars)

Harambee Stars hawajawahi kukutana na Gambia katika mechi ya mashindano yoyote ya kimataifa, jambo linalofanya mchezo wa leo kuwa wa kuvutia zaidi kwani mataifa yote mawili yanatafuta kuboresha nafasi zao katika kundi hili.

Kenya inashika nafasi ya nne ikiwa na pointi tano, huku Gambia ikiwa ya tano na pointi tatu.

Mara ya mwisho kwa Harambee Stars kushinda ugenini katika mechi ya kufuzu kwa Kombe la Dunia ilikuwa ya Oktoba 7, 2015 waliposhinda dhidi ya Mauritania 5-2 huko Port Louis.

Gambia inashika nafasi ya 125 katika viwango vya FIFA, wakati Kenya iko katika nafasi ya 108.

Hii itakuwa ni mechi ya kwanza kwa kocha mpya wa Harambee Stars, Benni McCarthy kutoka Afrika Kusini.

McCarthy, ambaye alishinda Ligi ya Mabingwa ya Ulaya na Porto mwaka 2004, alikubali kuwa kocha wa Kenya tarehe 3 Machi.

Kocha wa Gambia, Johnathan McKinstry, amekuwa katika wadhifa huo kwa miaka miwili. Pia ameahi kuifundisha McKinstry Gor Mahia kati ya Julai 2022 hadi Mei 2024 na kushinda mataji mawili ya ligi na ameeleza kuwa atatumia ujuzi wake kuhusu soka la Kenya kuishinda Harambee Stars.

Mchezaji wa Gambia ambaye anaitumikia ligi ya Tanzania akiwa na klabu ya Azam FC, Gibril Sillah, atakutana ndugu zake wa Kenya wanakipiga Tanzania kama Duke Abuya anayeitumikia Yanga na Elvis Rupia anayekipiga Singida Black Stars.

McCarthy anategemea wachezaji wa Kenya walioko nje ya nchi. Kikosi chake cha wachezaji kinajumuisha wachezaji wanne tu wa nyumbani: Rooney Onyango (Gor Mahia), Farouk Shikalo (Bandari), Mansur Okwaro (KCB), Mohamed Bajeber (Kenya Police) na Ben Stanley (Gor Mahia)

Timu ya Taifa Gambia

.

Mshambuliaji wa timu ya Al Duhail ya Qatar, Michael Olunga, atakuwa kiongozi wa mashambulizi ya Kenya.

“Kocha mpya ana imani nasi na tunatarajia mechi hii. Gambia ni timu inayoinukia na ina kikosi kizuri, hivyo lazima tutumie bora yetu,” alisema nahodha wa Harambee Stars, Michael Olunga. “Kwa maandalizi mazuri tuliyokuwa nayo, tutashuhudia matokeo mazuri kutoka kwa wachezaji vijana katika timu,” aliongeza Olunga.

 Viongozi wa kundi, Ivory Coast, wanashika nafasi ya kwanza kwa pointi 10, wakifuatiwa na Gabon (9) na Burundi (7).

  • Makipa: Ian Otieno, Brian Bwire, Farouk Shikalo
  • Walinzi: Johnstone Omurwa, Brian Mandela, Daniel Anyembe, Amos Nondi, Erick Ouma, Manzur Okwaro, Ronny Onyango
  • Viungo: Anthony Akumu, Richard Odada, Gonzalez Ismael, Timothy Ouma, Eric Johana, Duke Abuya, Mohamed Bajaber, Ben Stanley Omondi
  • Washambuliaji: Masoud Juma, Jonah Ayunga, Elvis Rupia, John Avire, Michael Olunga.
  • GOLIKIPA: Ebrima Jarju, Sheikh Sinyan, Musa Dibaga
  • MABEKI: Omar Colley, Omar Gaye, Lars Joseph Ceesay, Dadi Dodou Gaye, Momodou Lion Njie, Sheriff Sinyan
  • VIUNGO: Saikou Touray, Ebrima Adams, Abubakr Barry, Alasana Manneh, Mahmudu Bajo, Ebrima Darboe, Ablie Jallow
  • WASHAMBULIAJI: Musa Barrow, Alieu Fadera, Gibril Sillah, Yankuba Minteh, Abdoulie Sanyang,  Ali Sowe, Abdoulie Ceesay, Alassana Jatta

TAKWIMU ZA MASTAA WA LIGI KUU

Related Posts