Aucho, Dube mambo magumu, Diarra kicheko

Kuanzia Jumatano, Machi 19, 2025 hadi jana Alhamisi, nyota nane (8)  wanaocheza timu tofauti za Ligi Kuu Tanzania Bara wamekuwa wakizitumikia timu zao za taifa zinazoshiriki mashindano ya kuwania kufuzu fainali za Kombe la Dunia 2026.

Katika mechi zao hizo baadhi zimepata matokeo mazuri, nyingine zimeondoka na pointi moja moja na kuna zilizoangusha pointi zote tatu.

Matokeo hayo ya mechi hizo yamekuwa na faida kwa baadhi ya timu kwenye makundi yao ya kuwania kufuzu Fainali za Kombe la Dunia lakini kuna ambazo zimeathirika.

Mwananchi Digital imefuatilia kile ambacho kimefanywa na nyota wa timu za Ligi Kuu Tanzania Bara katika harakati za kupambania tiketi ya kushiriki Kombe la Dunia na kile ambacho timu zao za taifa zimevuna.

Khalid Aucho & Steven Mukwala

Kiungo wa Yanga, Khalid Aucho amekuwa nahodha wa Uganda katika mchezo wake iliocheza ugenini huko Misri dhidi ya Msumbiji ambapo timu yake imepoteza kwa mabao 3-1.

Hakuwa peke yake kwani hata mshambuliaji wa Simba, Steven Mukwala aliyeingia

Matokeo hayo yameifanya Msumbiji ikwee hadi kileleni mwa msimamo wa kundi G ikifikisha pointi 12 huku Uganda ikibakia katika nafasi ya tano na pointi zake sita.

Kiungo wa tabora United, Banele Sikhondze amecheza kwa dakika 84 katika mechi ambayo timu yake ya taifa ya Eswatini imetoka sare tasa nyumbani na Cameroon.

Sare hiyo imeipa pointi ya kwanza Eswatini inayioshika mkia katika kundi D.

Kenya imepambana na kusawazisha mabao matatu katika mchezo dhidi ya Gambia ulimalizika kwa sare ya mabao 3-3 ukiwa ni mchezo wa kundi F.

Duke Abuya wa Yanga aliingia katika dakika ya 70 kuchukua nafasi ya Richard Odada na Elvis Rupia hakucheza katikia mechi hiyo ambayo imefanya Kenya kuwa nafasi ya nne kwenye kundi F ikiwa na pointi sita.

Aliitwa katika kikosi cha timu ya taifa ya Gambia kwa ajili ya mchezo dhidi ya Kenya na hakupata nafasi ya kucheza.

Gambia imetoka sare ya mabao 3-3 katika mchezo huo na kufikisha pointi nne.

Sare ya mabao 2-2 nyumbani dhidi ya Benin imeshindwa,kuitoa timu ya Zimbabwe mkiani mwa msimamo wa kundi C ikifikisha pointi tatu.

Katika mechi hiyo, Myota wa Yanga, Prince Dube alicheza kwa dakika 46 za kipndi cha kwanza na hakufumsnis nyavu.

Huku Diarra akiwa langoni, mali imepata ushindi mnono wa ugenini wa mabao 3-0 dhidi ya Comoro ambao umeisogeza hadi katika nafasi ya nne kwenye msimamo wa kundi I ikifikisha pointi nane.

Related Posts