Balile, Machumu wachukua fomu kutetea nafasi zao TEF

Dar es Salaam. Mwenyekiti wa Jukwaa la Wahariri Tanzania (TEF), Deodatus Balile leo Ijumaa, Machi 21, 2025 amechukua fomu ya kutetea nafasi hiyo katika ofisi za jukwaa hilo jijini Dar es Salaam.

Balile akisindikizwa na baadhi ya wanachama, amekabidhiwa fomu na Kaimu Ofisa Mtendaji Mkuu wa TEF, Anitha Mendioza. Mkutano mkuu wa uchaguzi unatarajia kufanyika Songea, Mkoa wa Ruvuma kuanzia Aprili 3-5, 2025.

Mwenyekiti wa Jukwaa la Wahariri Tanzania (TEF), Deodatus Balile.

Mgeni rasmi kwenye mkutano huo ni Katibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi (CCM), Dk Emmanuel Nchimbi ambaye pia ni mgombea mwenza wa urais katika Uchaguzi Mkuu wa Oktoba 2025.

Mbali na Balile, wagombea wengine wanaendelea kuchukua fomu akiwemo Bakari Machumu ambaye amechukua kutetea nafasi yake ya makamu mwenyekiti.

Makamu Mwenyekiti wa Jukwaa la Wahariri Tanzania (TEF), Bakari Machumu.

Nafasi ya ujumbe wa Kamati ya Utendaji (KUT) inatarajiwa kuwa na ushindani mkali kutokana na idadi kubwa ya wanaojitokeza tofauti na nafasi ya uenyekiti na umakamu.

(Imeandikwa na Mwandishi Wetu).

Related Posts