Afisa Mkuu wa Wateja Binafsi na Wateja Maalum wa Benki ya Stanbic Tanzania, Omari Mtiga, akiwa katika mazungumzo na Rais wa Kanda ya Ulaya ya Kati na Mashariki, Mashariki ya Kati na Afrika (CEMEA), Andrew Torre juu ya masuala mbalimbali yanayohusu VISA. Tukio limefanyika makao makuu ya benki ya Stanbic jijini Dar es salaam, alipotembelea benki hiyo kwa ajili ya majadiliano kuhusu Visa ili kuleta mageuzi katika mfumo wa malipo ya kidijitali, mikakati ya kuimarisha ujumuishi wa kifedha, na fursa za ushirikiano wa kimkakati ambayo yataleta mapinduzi katika sekta ya fedha nchini Tanzania.Afisa Mkuu wa Wateja Binafsi na Wateja Maalum kutoka Benki ya Stanbic Omari Mtiga akiwa katika meza ya mazungumzo na Uongozi wa Timu ya Visa Kikanda . Wengine katika picha kushoto ni Meneja wa kitengo cha Bima, Irene Mutahibirwa. Tukio hilo limefanyika jijini Dar es salaam.
