Kabila akutana na Mbeki waijadili Mgogoro wa DRC – Global Publishers



Joseph Kabila

Rais wa zamani Thabo Mbeki na Joseph Kabila walifanya mazungumzo katika Taasisi ya Thabo Mbeki huko Johannesburg juzi Jumatano, wakijadili uongozi wa Afrika na maendeleo na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Watu wa Kongo (DRC).

Mkutano kati ya viongozi hao wawili unafanyika baada ya mazungumzo ya Jamhuri DRC yaliyokuwa yakifanyika Luanda, Angola, kuvunjika. Mazungumzo hayo yalilenga kutafuta amani ya kudumu katika eneo la mashariki mwa DRC.

Vuguvugu la waasi wa M23 lilijiondoa kwenye mazungumzo hayo likidai kuwa baadhi ya wanachama wake waliwekewa vikwazo.

Mbeki alikuwa Mwenyekiti wa Umoja wa Afrika mwaka 2002 wakati Kabila na Rais wa Rwanda, Paul Kagame, waliposaini makubaliano ya amani huko Sun City, Afrika Kusini.

Hata hivyo, makubaliano hayo hayakutekelezwa. Kabila alisisitiza umuhimu wa suluhisho la kudumu kwa mgogoro wa mashariki mwa DRC, akisema kuwa juhudi za kidiplomasia lazima ziwe jumuishi na zizingatie maslahi ya wananchi wa Kongo. Alieleza kuwa amani haiwezi kupatikana bila kutatua mizizi ya mgogoro huo, ikiwa ni pamoja na ushawishi wa mataifa ya kigeni na masuala ya usimamizi wa rasilimali.

Pia alikumbusha kwamba makubaliano ya Sun City yalikuwa hatua muhimu, lakini kutotekelezwa kwake kumefanya hali kuwa mbaya zaidi.
Kabila alisisitiza kuwa Afrika inahitaji uongozi thabiti na mshikamano wa kweli ili kutatua migogoro yake kwa njia ya amani na maendeleo endelevu.











Related Posts