Tanzania Prisons hadi huruma Ligi Kuu

LIGI Kuu Bara ikiwa imesimama kwa muda kupisha kalenda ya FIFA, huku Yanga ikuiwa kileleni mwa msimamo ikiwa na pointi 58 na mabao 58 ya kufungwa, ikifuatiwa na Simba, hali ni mbaya kwa Tanzania Prisons, kwani yenyewe ndio timu yenye safu butu ya ushambuliaji katika ligi hiyo.

Maafande hao wanaoshikilia nafasi ya 15 katika msimamo juu ya waburuza mkia, KenGold katika mechi 23 ilizocheza hadi sasa imefunga mabao 12, ikiwa ndio timu inayoshika mkia kwa kufumani nyavu hadi sasa wakati zikiwa zimeshacheza jumla ya mechi 181 na kuzalisha mabao 406.

Prisons iliyokusanya pointi 18, mbili zaidi na ilizonazo KenGold inayoshiriki Ligi Kuu kwa mara ya kwanza yenye 16, imezidiwa na waburuza mkia hao, kwani wachimba dhahabu hao wamefunga mabao 20 hadi sasa kupitia mechi 23 pia.

Katika mechi 23 Prisons, imeshinda michezo minne tu, huku ikitoka sare sita na kupoteza 13 na imeruhusu mabao 31 na katika kuhakikisha timu inakaaa vyema ili kumalizia mechi saba za mwisho, mabosi wa klabu hiyo umeamua kuwarejesha wachezaji wakongwe, Salum Kimenya na Jumanne Elfadhil ili kusaidiana na wengine waliopo kambini kuiokoa timu.

Katibu wa Prisons, John Matei alikiri wachezaji hao wamejiunga na wenzao katika kambi ya siku 10 ambayo wameiweka katika chuo cha Magereza kilichopo Kiwira.

Matei aliyewahi  kuitumikia timu hiyo kuanzia msimu wa 2008 hadi 2015 alisema hata enzi akicheza, waliwahi kupitia nyakati ngumu kama ilivyo kwa sasa, lakini walipambana timu ikasalia Ligi Kuu.

“Msimu wa 2014-2015 zilibakia mechi nane tulikuwa na nyakati ngumu kama tulizonazo kwa sasa, tukashinda mechi tano, tukatoka sare mbili ikashuka Ruvu Shooting, kocha alikuwa Mbwana Makata, pia 2011-2012 timu ilishuka ikaja ikapanda msimu uliofuata,” alisema Matei.

Timu inayoifuata Prisons kwa kuwa na safu butu ya ushambuliaji ni Pamba Jiji iliyorejea katika Ligi Kuu baada ya kuisotea kwa miaka 23 tangu iliposhuka 2001, ikiwa imefunga mabao 14 katika mechi 23 ikiwa nafasi ya 13 kwenye msimamo, huku yenyewe ikifungwa mabao 25.

Timu za KMC na Namungo zinafuata katika orodh ya timu zilizofunga idadi ndogo ya mabao kila moja ikitupia 16 katika mechi 23 ilizocheza kila moja, zikifuata katika msimu moja ikiwa nafasi ya 11 na 12, ila zinatofautiana mabao iliyofungwa. KMC imefungwa 34 na Namungo 28.

Wakati vita ya watani wa jadi wakiachana kwa mabao sita, Azam FC inashikiria nafasi ya tatu kwenye upachikaji mabao ikiingia kambani mara 36, inafuata Singida Black Stars ambayo imefunga mabao 32.

Licha ya kukusanya pointi chache ikiwa nafasi ya saba nyuma ya Tabora United na JKT Tanzania Fountain Gate inashika nafasi ya tano kwenye upachikaji wa mabao ikifunga 28, Tabora United ipo nafasi ya tano kwenye msimamo lakini kwenye ufungaji imedondokea nafasi ya sita baada ya kufunga mabao 27.

Nafasi ya saba kwa upachikaji mabao inashikiliwa na Dodoma Jiji ambayo ipo nafasi ya nane kwenye msimamo imefunga mabaop 22, Mashujaa imefunga mabao 19, JKT Tanzania, Kagera Sugar na Coastal Union zote zimefunga mabao 18.

Timu nyingine zilizofunga mabao machache zaidi ni KMC ikiingia kambani mara 16 sawa na Namungo, Pamba Jiji wao wamefunga mabao 14.

Related Posts