ASMA MWINYI AFTARISHA WATU WA SURA MFANANO

Na Madina Khatib, Zanzibar

NAIBU Waziri ya maendeleo ya jinsia, wazee na watoto Zanzibar, Anna Athanas Paul, amesema taasisi ya Asma Mwinyi Foundation imekuwa na mchango mkubwa katika jamii hasa katika kuhakikisha kuwa haki za watoto na watu wenye ulemavu wakiwemo wenye sura mfanano zinaendelezwa na kuheshimiwa.

Akizungumza katika hafla ya Iftar iliyoendana na maadhimisho ya siku ya watoto wenye sura mfanano ( Down Syndrome) iliyoandaliwa na taasisi ya Asma Mwinyi Foundation katika viwanja vya Vuga Lebano.

Alisema, jukumu lake ni la kipekee na imeonekana athari chanya za juhudi zake katika kuhamasisha jamii ambapo hafla hiyo pia imeonesha mshikamano na kusaidia kuondoa mitazamo potovu na changamoto zinazowakabili.

Aidha alisema pamoja na kuadhimisha siku hiyo pia ni vyema kuenxi utu, haki na fursa kwa kila mtoto na mtu mwenye ulemavu kwani kila mmoja ana haki ya kuishi kwa heshima na kupata elimu, huduma na fursa sawa na wengine.

” Watu wenye sura mfanano ni sehemu ya jamii na wanapaswa kujivunia, kuthaminiwa na kuungwa mkono kwa kila hatua wanazozichukua” alisema.

Hivyo, wizara ya maendeleo ya jinsia, wazee na watoto wanathamini juhudi za serikai ya Mapinduzi ya Zanzibar katika kuimarisha huduma za afya, elimu na ustawi wa jamjj kwa watoto na watu wenye mahitaji maalum.

Sambamba na hayo, alisema wizara inaendelea kufanya kazi kwa karibu na wadau mbalimbali ili kuhakikisha kwamba haki za watoto wa kike na kiume hasa wale wenye mahitaji maalum ya aina mbalimbali zinatambuliwa na kuzingatiwa katika sera na mipango ya maendeleo.

Kwa upande wake Mkurugenzi wa Taasisi ya Asma Mwinyi Foundation, Asma Ali Hassan Mwinyi, alisema wataendelea kuwaunga mkono watoto hao na kuendelea kuthamini kwani wanaendelea kuunga mkono.

Hata hivyo, alisema, taasisi yake itaendelea kushirikiana na wadau mbalimbali ili kuona watoto hao nao wanahitaji masuala mbalimbali.



Related Posts