BALOZI NCHIMBI MSIBANI KWA HAWASSI

Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Balozi Dkt. Emmanuel John Nchimbi, akiwa kwenye msiba wa Bi. Damaris Simeon Hawassi, aliyekuwa mke wa Katibu wa Halmashauri Kuu ya CCM Taifa (NEC), Uchumi na Fedha, Dkt. Frank Haule Hawassi, nyumbani kwa marehemu, eneo la Mihuji, jijini Dodoma, leo Jumamosi, tarehe 22 Machi 2025.

Mbali na kusaini kitabu cha maombolezo na kumfariji Dkt. Hawassi, Balozi Nchimbi, akiwa na viongozi wengine waandamizi na wastaafu wa Chama na Serikali, alipata wasaa wa kutoa heshima za mwisho.


Related Posts