Papa kufundishwa kuzungumza, kisa oksijeni – Global Publishers

VATICAN CITY, VATICAN – AUGUST 09: (EDITOR NOTE: STRICTLY EDITORIAL USE ONLY – NO MERCHANDISING). Pope Francis attends his weekly General Audience at the Paul VI Hall on August 09, 2023 in Vatican City, Vatican. Following his traditional July break, Pope Francis resumed his weekly General Audiences, and reflected on his recently-concluded Apostolic Journey to Portugal for World Youth Day in Lisbon. (Photo by Vatican Media via Vatican Pool/Getty Images)

Kiongozi wa Kanisa Katoliki, Papa Francis, baada ya kuwa kitandani kwa zaidiya wiki sita sasa analazimika “kujifunza tena kuzungumza” kutokana na athari za matumizi ya muda mrefu ya oksijeni yenye mtiririko mkubwa, Kardinali Victor Manuel Fernandez amesema.

Kardinali huyo, ambaye ni mkuu wa ofisi ya mafundisho ya imani ya Vatican, amekanusha uvumi kwamba Papa anafikiria kujiuzulu, akisema anarejea katika hali yake ya kawaida.

“Papa yuko vizuri sana, lakini oksijeni yenye mtiririko mkubwa hufanya koo kukauka sana. Anahitaji kujifunza tena jinsi ya kuzungumza, lakini hali yake ya jumla ya mwili iko kama ilivyokuwa hapo awali,” alisema Fernandez wakati wa uzinduzi wa kitabu kipya cha Papa kuhusu ushairi.

Papa Francis, mwenye umri wa miaka 88, amesikika mara moja tu hadharani tangu alazwe, kupitia rekodi ya sauti iliyotolewa na Vatican Machi 6. Mwaka huu na Sauti yake ilikuwa dhaifu, ilikatikakatika na haikuwa rahisi kueleweka.

Katika taarifa ya hivi karibuni kutoka Vatican, imethibitishwa kuwa afya yake inaendelea kuimarika polepole, huku akionesha maendeleo madogo katika kupumua na kutembea. Vatican imesema tangu Jumatatu, hajatumia mashine ya kusaidia kupumua usiku, bali anapokea oksijeni kupitia kibomba kidogo puani kwa muda mwingi wa mchana.

Bado hakuna tarehe rasmi iliyotolewa kuhusu lini Papa ataruhusiwa kuondoka hospitalini. Kardinali Fernandez amesema hajui ikiwa Papa atarejea Vatican kabla ya Pasaka, itakayoadhimishwa Aprili 20, lakini madaktari wanataka kuwa na uhakika wa asilimia 100 kabla ya kumruhusu.

Alipoulizwa kuhusu uwezekano wa Papa Francis kujiuzulu, Kardinali Fernandez alijibu kwa mkato: “Sidhani kabisa, hapana.”

Related Posts