Na Mwandishi Wetu,Kagera
MAKAMU Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Tanzania Bara, Stephen Wasira amewasili mkoani Kagera kuanza ya kikazi ya siku nne.
Wasira amepokelewa leo Machi 22, 2025 katika Uwanja wa Ndege wa Bukoba akiwa ameongozana na viongozi mbalimbali wakiwemo baadhi ya wajumbe wa Halmashauri Kuu ya Taifa (NEC) ya CCM.
Ziara hiyo ina lengo la kukagua uhai wa Chama, utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi ya CCM ya 2020-2025, kusikiliza changamoto za wananchi pamoja na kuhutubia mikutano ya hadhara ambapo katika siku ya kwanza atahutubia mkutano mkubwa Kata ya Kemondo, Wilaya Bukoba.