KITABU CHA MAISHA YA OMWAMI KASHAGA CHAZINDULIWA.


Mgeni rasmi, Profesa wa Historia kutoka Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Frederick Kaijage akikata utepe kuzindua kitabu kiitwacho ‘Maisha ya Omwami Evarista Kashaga’ jijini Dar es Salaam Machi 22, 2025. Kulia ni Mwandishi wa kitabu hicho, Mhadhiri Mwandamizi wa Sayansi za Jamii kutoka Chuo Kikuu cha Kimataifa cha Kampala, Dkt. Frateline Kashaga, Mtaalam mstaafu wa Uchumi, Adelaide Lukaija (kushoto) na mashuhuda wengine. (Picha na Robert Okanda)

Mwandishi wa kitabu hicho, Mhadhiri Mwandamizi wa Sayansi za Jamii kutoka Chuo Kikuu cha Kimataifa cha Kampala, Dkt. Frateline Kashaga akizungumza na waalikwa katika uzinduzi wa kitabu hicho. Wa pili kushoto ni mgeni rasmi, Profesa wa Historia kutoka Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Frederick Kaijage na Mtaalam mstaafu wa Uchumi, Adelaide Lukaija.

Wajukuu wa Omwami Evarista Kashaga wakishiriki katika uzinduzi wa kitabu hicho.

Baadhi ya wageni waalikwa wakifuatilia matukio katika uzinduzi wa kitabu cha Omwami Evarista Kashaga

Mgeni rasmi, Profesa Frederick Kaijage (wa pili kushoto)akiwa na baadhi ya washiriki bada ya kuzindua kitabu hicho.

Baadhi ya wageni waalikwa wakifuatilia matukio katika uzinduzi wa kitabu cha Omwami Evarista Kashaga

Mgeni rasmi, Profesa Frederick Kaijage (wa pili kushoto)akiwa na baadhi ya washiriki bada ya kuzindua kitabu hicho.

Na Mwandishi Wetu

PROFESA wa Historia kutoka Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM) mstaafu, Frederick Kaijage, ametoa rai kwa jamii kujenga utaratibu wa kuandika vitabu kuhusu yao, ili kuweka historia kwa vizazi vyao vijavyo.

Prof. Kaijage, mwanataaluma mbobevu wa historia, aliyasema hayo mwishoni mwa wiki, wakati wa kuzindua kitabu kiitwacho; ‘Maisha ya Omwami Evarista Kashaga’, jijini Dar es Salaam.

“Duniani kwa watu kuna kitu tunaita utambulisho, ndio kitu muhimu. Kwa sababu wewe ukiwa hapa (duniani), unafikiri wewe ni nani? Umetoka wapi? Watu wanoishi na ambao wamekwishaondoka una uhusiano gani nao?

“Jaribu kujielewa wewe mwenyewe chimbuko lako, kitu kinachokutambuliosha ni kitu kipi. Mimi naweza kujitambulisha ni Profesa, maana yake nini? Sawa kwa wanataaluma wenzangu.

“Wataona ni muhimu sana. Lakini mimi ni mtoto wa Kaijage, huo ni utambulisho zaidi kuliko vitu vilivyokuja baadae, historia yao, jitambue, jielewe, jitambulishe,” alisema Prof. Kaijage.

Alisema kujitambua ndio msingi wa watu kutambuana na kwamba koo mbalimbali zilizomo duniani si kitu cha kugawiwa bali huendana na vinasaba vya jamii ya kundi fulani.

“Vinasaba vyako ndio wewe, ndio vinasadifu ukoo wako. Kuna sehemu ukitembea utakutana na koo fulani. Kuandika kuhusu koo fulani si kwamba ni ukabila, ni kwa lengo la kutambuana, mshikamano na upendo. Utaifa utatambulishwa na wahusika, ila kuhusu ukoo ni wewe mwenyewe,” aliongeza mwanataaluma huyo.

Naye Mwandishi wa Kitabu hicho, Mhadhiri Mwandamizi wa Sayansi za Jamii kutoka Chuo Kikuu cha Kimataifa cha Kampala, Dkt. Frateline Kashaga, alisema lengo la uandishi wa kitabu hicho ni kutunza kumbukumbu kwa kuwa walio wengi hutunza historia zao kwa hadithi.

Alibainisha kuwa Watanzania wenye nia ya kutunza historia vitabuni, hata kwa mfumo wa kisasa kidijitali bado hukumbwa na changamoto kadhaa ikiwamo uchumi duni. Mathalani mzee wa Ukoo, Evarista Kashaga alifanya mambo makubwa sana, kipindi cha ukoloni chini ya Gavana wa Kiingereza na WaAfrika hawakuwa na haki sawa za kisiasa, kiuchumi na kitamaduni ikilinganishwa na jamii ya Waasia, Warabu na Wazungu.

Aliongeza sababu muhibu ya uandishi wa kitabu hicho ni kutunza mila na desturi za Ukoo wetu ambao ulibebwa na Mzee Evarista Kashaga kama nembo ya Ukoo.

“Pamoja na changamoto zilizopo kutunza kumbukumbu za familia ni utamuduni mzuri. Kuhusisha watafiti, wataalamu wa lugha, wadau wa ili kufadhili, itafanikisha hilo, kusaidia jamii zetu kuacha urathi,” alisema Dk. Kashaga.

Related Posts