Shule ya Sekondari Green Acres kutumia nishati mbadala




Na mwadishi Wetu.

Katika jitihada za kuunga mkono juhudi za Rais wa awamu ya Sita Dk.Samia Suluhu Hassan za kuhifadhi mazingira Shule ya Green Acres ya Mbezi Beach Dare s Salaam sasa inajipanga kutumia nishati mbadala katika matumizi ya kupikia shuleni hapo.

Mwalimu Mkuu wa Shule hiyo Jonathan Kasabila alisema kuwa shule hiyo ilifanya upembuzi yakinifu ili iweze kutumia nishati hiyo.

“Tumeshaongea na wataalam wa mradi huo ili hatimaye tuweze kutumia nishati mbadala tutaanza na makaa ya mawe na kisha Bio gas (nishati Itokanayo na kinyesi) na kwamba tunafanya haya kwa lengo la kuiunga mkono serikali ambayo inatutaka tututmie nisha ya aina hiyo,” alisema

Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Dk. Doto Biteko alisema kuwa katika mwaka 2024/25 Serikali itaendelea kutekeleza hatua madhubuti za kuimarisha matumizi ya Nishati Safi ya kupikia nchini.

Alisema hayo Aprili 24, 2024 bungeni jijini Dodoma wakati akiwasilisha Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Wizara ya Nishati kwa Mwaka 2024/25.

Shule ya Sekondari ya Green Acres ipo Mbezi Beach kata ya Wazo Wilaya ya Kinondoni na ina toa elimu kuanzia kidato cha kwanza hadi ha sita na imekuwa ikifaya vizuri katika matokeo ya mitihani ya kitaifa kwa muda Mrefu sasa.

Shule hiyo ya sekondari ya Mchepuo wa Kiingereza inampongea Rais Samia kwa kutimiza miaka minne madarakani.

“Amefanya mambo makubwa sana Rais wetu, amejenga shule nyingi za watoto wa kike, amejenga zahanati za kutosha hapa nchini, wewe ni shahidi angalia miundombinu inavyojengwa hapa nchini,” alisema.

Kuhusu sera mpya ya elimu, anasema kwamba serikali imefanya jambo jema kuleta sera hiyo,kwa ni inawasaidia vijana kujiajiri pindi watakapomaliza masomo yao.

alisema shule ina shirikiana na serikali kwa kutekeleza miongozo mbalimbali ikiwamo sera mpya ya elimu.

Alisema sera hiyo ambayo inatilia mkazo mafunzo kwa vitendo kwa wanafunzi inajenga msingi mzuri kwa wanafunzi kujiajiri pindi wamalizapo masomo yao.

Alisema kupitia sera hiyo watoto wanafundishwa standi mbalimbali za kazi mfano Tehama,kilimo, upishi, ushonaji na muziki.

“Sisi hapa tuna darasa la Tehama, tumeanza nayo hiyo, tunaendelea vizuri na darasa hilo hilo la mafunzo kwa vitendo na tunategemea kuendelea na stadi nyingine za kazi muda unavyokwenda.

“Nitoe rai kwa wazazi kuwaleta watoto wao hapa kwa ajili ya elimu ya darasani na pia kupata ujuzi wa fani mbalimbali,” Anasema wana waalimu wazuri, mazingira mazuri ya kusomea na maabara kwa ajili ya masomo ya sayansi kwa vitendo .

Mazingira ya shule na wanafunzi

Uwanja wa mpira wa shule
 

Related Posts