MADIWANI WA ARUSHA WAKATAA KUGAWA JIMBO LA ARUSHA MJINI



Na Pamela Mollel,Arusha

MADIWANI wa Halmashauri ya jiji la Arusha wakubaliana kwa pamoja kutogawa jimbo la Arusha mjini mara mbili, badala yake wamekubaliana kugawanywa kwa kata nane za jiji hilo.
Taarifaa hizi zinakuja wakati mwafaka kuelekea uchaguzi mkuu ambapo hivi karibu zimekuwepo kwa taarifa zisizorasmi zikidai jimbo hili kugawanywa mara mbili kutoka na ukubwa wake
Leo Machi 25 ,2025 Madiwani wamevunja ukimya kwa kukataa kwa pamoja madai ya kuugawa jimbo Arusha kwa madai kuwa halina ukubwa wa kutisha katika kuwahudumia wananchi
Akizungumza na waandishi wa habari Jijini Arusha,mara baada ya kumalizika kwa baraza maalum la Madiwani,Meya wa jiji Maxmillian Iranqhe anasema kuwa walichokubaliana katika kikao hicho ni kugawanywa kwa kata nane tu,ambazo zimeonekana kuna changamoto katika kuwafikia wananchi na kushindwa kutatua kero kwa wakati kutokana na ukubwa wa eneo
“Mpaka sasahivi tulichokubaliana zigawanywe kata hizo nane na tumefanya hivyo ili kuharakisha maendeleo katika kata husika ili kuweza kutatua kero kwa wananchi “Anasema Iranqhe
Aidha ameongeza kuwa Madiwani wamepitisha kata ya Muriet,Moshono,Sokoni1,Sinoni,Lemara na Terat
Kwa upande wake diwani wa kata ya Sakina Vicent Willson anasema kugawanywa kwa kata hizo ni mapendekezo kutoka kwa baadhi ya madiwani wa kata hizo ambazo zinaonyesha changamoto wanazokutana nazo katika kuwahudumia wananchi kutokana na ukubwa wa eneo.
“Jimbo la Arusha lina ukubwa wa kilometa za mraba 272 hatujaona sababu za msingi za kuugawa ila kwenye kata ni Sawa maana kuna kata zingine ni kubwa sana inabidi utembee umbali mrefu katika kuwahudumia wananchi”Anasema Willson

Related Posts