Mjumbe Maalum wa Rais wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, Mhe. Antonie
Tshisekedi ambaye pia ni Waziri wa Mambo ya Nje wa nchi hiyo Mhe.
Therese Kayikwamba Wagner amewasili nchini.
Katika Uwanja wa
Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere, jijini Dar es Salaam Mhe. Wagner
amelakiwa na Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano na Afrika
Mashariki anayeshughulikia masuala ya Afrika Mashariki, Mhe. Dennis
Londo.
Akiwa nchini Mhe. Wagner anatarajia kuwasilisha
ujumbe maalum wa Mheshimiwa Rais Tshisekedi kwa Rais wa Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan.
Waziri wa mambo ya Nje wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo Mhe.
Therese Kayikwamba Wagner akiwasili katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa
wa Julius Nyerere jijini Dar es Salaam
Waziri wa mambo ya Nje wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo Mhe. Therese
Kayikwamba Wagner (kushoto) amepokelewa na Naibu Waziri wa Mambo ya Nje
na Ushirikiano wa Afrika Mashariki anayeshughulikia masuala ya Afrika
Mashariki Mhe. Dennis Londo.