NMB Yadhamini na Kushiriki Uzinduzi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru 2025

Na mwandishi weru

Leo Aprili 02, 2025, Benki ya NMB imedhamini na kushiriki uzinduzi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru 2025 kitaifa uliofanyika katika viwanja vya Shirika la Elimu Kibaha, mkoani Pwani.

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango, ameuwasha rasmi Mwenge wa Uhuru mbele ya Waziri Mkuu, Mhe. Kassim Majaliwa Majaliwa, na viongozi wengine wa Serikali. Baada ya uzinduzi huo, Dkt. Mpango amekabidhi Mwenge wa Uhuru kwa Kiongozi wa Mbio za Mwenge Kitaifa kwa mwaka 2025, Ismail Ussi.

Ussi ameahidi kuukimbiza Mwenge huo katika halmashauri 165 kwenye mikoa yote 31 nchini, kwa kauli mbiu inayohimiza wananchi kushiriki kikamilifu katika Uchaguzi Mkuu kwa amani na utulivu.

Benki ya NMB, ikiwakilishwa na Meneja wa Kanda ya Dar es Salaam, Seka Urio, inaendelea kuwa mdau muhimu katika matukio ya kitaifa yenye lengo la kuhamasisha amani, mshikamano, na maendeleo.



Related Posts