Watu Saba Wafariki, 32 Wajeruhiwa Baada ya Basi Kupinduka Mwanga – Video – Global Publishers



Watu Saba wamefariki dunia papo hapo huku wengine 32 wakijeruhiwa baada ya basi la Kampuni ya Mvungi, walilokuwa wakisafiria kupinduka katika eneo la Kijiji cha Mamba, Kata ya Msangeni, Tarafa ya Ugweno, Wilaya ya Mwanga, mkoani Kilimanjaro.

Kamanda ya Jeshi la Zimamoto na Uokoaji mkoani Kilimanjaro, Jeremiah Mkomagi amethibitisha kutokea kwa vifo hivyo, ambapo amesema ajali hiyo imetokea leo Alhamisi saa moja asubuhi, ambapo basi hilo lilikuwa likitoka Ugweno kwenda mkoani Dar es salaam.

Amesema waliofariki katika ajali hiyo ni wanawake watatu akiwemo mtoto mdogo na wanaume wanne.

Akizungumzia tukio hilo la ajali, Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro, Nurdin Babu amesema chanzo cha ajali hiyo ni basi hilo lilikuwa likijaribu kupishana na gari jingine na ndipo lilipoteleza kwenye tope na kupindika.











Related Posts