China Yaikomoa Marekani Yapandishaushuru – Global Publishers



China imeikomoa Marekani kwani imetangaza kuwa itaanza kutoza ushuru wa asilimia 34 kwa bidhaa zinazoagizwa kutoka Marekani kuanzia Aprili 10, 2025. Hatua hiyo imekuja kama majibu kwa ushuru wa kiwango hicho hicho uliotangazwa na Rais wa Marekani Donald Trump mapema wiki hii dhidi ya bidhaa kutoka China.

 

Ushuru huo mpya unaongeza mzigo kwa bidhaa za China ambazo tayari zilikumbwa na ushuru mwingine, hivyo kufanya jumla ya ushuru kufikia asilimia 54 dhidi ya bidhaa za China zinazoingia Marekani.

 

Wizara ya Biashara ya China mjini Beijing imelaani hatua hiyo na kusema tayari imefungua kesi dhidi ya Marekani katika Shirika la Biashara Duniani (WTO) ikipinga ushuru huo wa upande mmoja wa Marekani.

 

Mbali na hilo, China pia imetangaza vizuizi vipya vya usafirishaji wa madini adimu, yanayotumika katika teknolojia kama vile chipu za kompyuta na betri za magari ya umeme (EV) — hatua inayolenga kuathiri moja kwa moja sekta muhimu za teknolojia ya Marekani.


Related Posts