***
Mwandishi wa habari wa siku nyingi, Rahabu Fredy aliyekuwa Mhariri Mkuu Msaidizi wa Idara ya Habari na Matukio katika kituo cha habari cha Azam Media, amefariki dunia leo April 5, 2025 akiwa anapatiwa matibabu katika Hospitali ya Muhimbili jijini Dar es Salaam.
Kwa mujibu wa chanzo cha karibu, Rahabu aliyekuwa mke wa aliyekuwa mtangazaji mahiri, marehemu Fred Fidelis almaarufu Fredwaa, alikuwa amelazwa kwa siku kadhaa kutokana na maradhi yaliyokuwa yakimsumbua.
Enzi za uhai wao, Rahabu na Fredwaa walipata umaarufu mkubwa wakiwa wanafanya kazi katika Kituo cha Radio Free Africa jijini Mwanza kabla ya kuhamia jijini Dar es Salaam.
Azam Media imethibitisha taarifa za Rahabu kufariki dunia.