******
Jukwaa la Wahariri Tanzania (TEF),limekamilisha safu ya uongozi wa Kamati ya Utendaji (KUT),baada ya wagombea 12 kuchaguliwa na kubakia saba.
Mapema mchana wajumbe wa mkutano huo 153 walitangaziwa na Mwenyekiti wa Kamati ya Uchaguzi,Frank Sanga ambaye aliwatangaza Mwenyekiti Deodatus Balile na Makamu wake,Bakari Machumu baada ya kuwa wagombea pekee wa nafasi hizo.
Hatua hiyo ni kutokana kulikosekana pingamizi kwa mujibu wa kanuni,jambo linaloipa mamlaka kamati kuwatqngqza wagombea pekee kuwa washindi wa nafasi hizo.