Kocha Fountain Gate Princess aitaka nafasi ya nne

KOCHA Mkuu wa Fountain Gate Princess, Camil Mirambo amesema malengo ya timu hiyo msimu huu ni kumaliza katika nafasi ya nne kwenye msimamo wa ligi.

Timu hiyo iko nafasi ya saba kwenye msimamo na katika mechi 13, imeshinda nne, sare mbili na kupoteza saba ikikusanya pointi 14.

Akizungumza na Mwanaspoti, Mirambo alisema wana nafasi ya kumaliza nafasi ya nne kwenye msimamo licha ya ugumu wa mechi tano zilizosalia na timu wanazowania nafasi hiyo.

“Tunatamani kumaliza nafasi ya nne lakini timu kama Alliance na Ceasiaa wanaipambania pia, Ceasiaa ndio walikuwa na mwendo mzuri lakini suluhu yao na Gets program inaonyesha hii nafasi inawezekana kwetu,” alisema na kuongeza;

“Muhimu ni kushinda michezo yetu, tunajaribu kuweka mpango mzuri wa uchezaji ili tufikie lengo, Fountain  niakademi ambayo imetoa vipaji vingi na kama kocha natamani kuendeleza timu ilipoishia msimu uliopita.”

Msimu uliopita timu hiyo ilimaliza nafasi ya tano na katika mechi 18, ilishinda saba, sare tano na kupoteza sita na pointi 26.

Related Posts