Kuitwa tena Taifa Stars hawa kazi ipo

TIMU ya Taifa ya Tanzania ‘Taifa Stars’ iliyoshiriki fainali za mataifa ya Africa (Afcon) za Ivory Coast ilikuwa na wachezaji wanaocheza soka la kulipwa katika mataifa mbalimbali Africa, Amerika, Asia na Ulaya katika ligi mbalimbali kubwa na ndogo.

Katika wachezaji hao ambao wengi wao walikuwa ni wageni machoni mwa Watanzania, walisubiriwa kuona watafanya nini katika kuibeba Stars kuanzia michezo ya kufuzu hadi ilipotinga katika fainali hizo, baada ya kuonyesha viwango katika timu zao na kusababisha kuitwa timu ya taifa.

Hata hivyo, wapo baadhi ambao baada ya fainali hizo, walikuwa na mwendelezo mzuri na kujikuta wakiitwa mara kwa mara akiwamo Haji Mnoga, Charles Mmombwa, huku wengine wakishindwa kurejea kutokana na kushindwa kucheza katika klabu zao au kukosa nafasi mara kwa mara.

Mwanaspoti linakuletea wachezaji hao ambao ni raia wa Tanzania lakini walizaliwa na kukulia nchi nyingine na baada ya kuitwa kwa mara ya kwanza Stars, wameshindwa kurudi kutokana na viwango vyao kushuka.

KUIT 01

Nyota huyo Mtanzania aliyezaliwa na kukulia Sweden aliitwa mara ya kwanza timu ya taifa Kufuzu Kombe la Dunia akianzia benchi kwenye mchezo dhidi ya Niger Novemba 18, Tanzania ikishinda bao 1-0.

Mchezo uliofuata Kawawa alianza na kumaliza dakika 90 dhidi ya Morocco licha ya kuruhusu mabao 2-0, lakini kipa huyo alionyesha kiwango bora kiasi cha kutabiriwa huenda akampa changamoto Aisha Manula.

Mara ya mwisho kuitwa Stars ilikuwa Juni 02 na tangu hapo makipa wengine kama Aboutwalib Mshery, Yona Amos, wamekuwa wakiitwa kwenye timu hiyo.

Kipa huyo kwa sasa anakipiga IFK Haninge Ligi daraja la pili nchini Sweden akitokea Syrianska FC alikocheza msimu mmoja na mechi moja.

Haninge imecheza mechi mbili za ligi ukiwa ni msimu mpya, huu Mtanzania huyo akianzia benchi.

Diallo mzazi wake mmoja ni Mtanzania huku mwingine ni Mholanzi ambako ndiko alizaliwa na kukulia.

Aliitwa kwa mara ya kwanza Januari 07 kwenye michezo ya kimataifa ya kirafiki dhidi ya Misri, Bulgaria, Sudan na Indonesia akicheza na kuonyesha uwezo mkubwa kama kiungo mchezeshaji.

Baada ya hapo mechi mbili za kufuzu AFCON dhidi ya Morocco na Zambia mwaka jana kiungo huyo aliambulia benchi akikutana na upinzani kutoka kwa Novatus Miroshi, Himid Mao na Adolf Mtasingwa ambao wamekuwa wakicheza eneo hilo.

Kiungo huyo anakipiga Eindhoven FC inayoshiriki Ligi Daraja la Kwanza Netherland akitokea Orebro Syr ya Sweden alikocheza kwa msimu mmoja.

Ikiwa imefikia raundi ya 32 ya ligi hiyo, kiungo huyo hajacheza mchezo wowote tangu atue kikosini hapo kwenye mechi tisa zilizochezwa.

KUIT 02

Beki huyo wa pembeni mama yake mzazi ni mzaliwa wa Kilimanjaro Tanzania na baba yake ni Muingereza, alizaliwa na kukulia England.

Mara ya kwanza kuitwa beki huyo ni mwaka 2019 kwenye kikosi cha timu ya taifa ya vijana U-17, Serengeti Boys kwenye fainali za Mataifa ya Afrika (AFCON).

Mara ya mwisho kiungo huyo kuonekana uwanjani na uzi wa Stars ni June 02 akiingia kutokea benchi kwenye mechi ya kimataifa ya kirafiki dhidi ya Indonesia iliyoisha kwa suluhu.

Tangu hapo hakuwa na timu baada ya kumaliza mkataba na Ilkeston na hakuitwa kwenye kikosi cha Stars kilichofuzu kucheza Afcon mwaka huu, Morocco.

Anaitumikia Harborough Town FC ya England inayoshiriki Ligi daraja la tatu lakini wakati ligi hiyo imetamatika hivi karibuni Starkie amecheza mechi mbili kwa dakika zote 90.

Starkie kabla ya kujiunga na timu hiyo, alichezea klabu mbalimbali ikiwemo Leicester City ya vijana, Wilhelmshaven, Shepshed Dynamo, Spalding United, Basford United, Alfreton Town na Ilkeston Town.

Hajaitwa muda mrefu timu ya taifa lakini akiwa na kikosi cha Boreham Wood ya England nyota huyo anaendelea kuaminiwa na kupewa nafasi.

Mtanzania huyo aliyezaliwa Somalia ukiwa ni msimu wake wa pili kuitumikia timu hiyo inayoshiriki Ligi daraja la kwanza England, msimu huu amecheza mechi 14 kwa dakika 1317.

KUIT 03
KUIT 03

Mei 19 ilikuwa mara ya mwisho kwa kiungo huyo mzaliwa wa England kuonekana na uzi wa Stars kwenye mechi ya kirafiki dhidi ya Sudan akianzia benchi.

Tangu hapo hajaitwa kwenye kikosi cha Stars lakini kwenye klabu anayoichezea ndio chaguo la kwanza la kocha kwenye eneo la kiungo.

Alijiunga na Rochdale ya England akitokea Wealdstone ya nchini humo na amecheza mechiu 35 za mashindano yote akifunga mabao manne.

KUIT 04

Ni miongoni mwa wachezaji walioitwa na kocha wakati ule, Adel Amrouche kufuzu kwa fainali za Mataifa ya Afrika mwaka jana.

Anakipiga Forfar Athletic inayoshiriki Ligi daraja la nne uscottish kama beki wa kati kwenye kikosi hicho.

Ukiwa msimu wake wa tatu kuitumikia timu hiyo, amekuwa mchezaji muhimu kwenye kikosi hicho akianza na kuonyesha kiwango kikubwa akicheza dakika 1960 kwenye mechi 22.

Related Posts