Wakazi waliokuwa Magomeni Kota wamepinga mkataba wa Sm Mpangaji mununuzi ulioandaliwa kwa upande wa Serikali kupitia Wizara ya Ujenzi baada ya kubaini kiwepo kwa mapungufu ya kisheria na kiutekelezaji na kutaka majadiliano kwa pande mbili.
Mkataba wa upqngaji ununuzi linatokana na maamuzi yaliyotokana kwa pande mbili hivyo kwa sasa tangu kuingia katika nyumba zilizojengwa na TBA na kuhamia pamekosekona ushirikiano thabiti.
Akizungumza katika mkutano wakazi wa Magomeni Kota nyumba mpya za TBA Katibu wa Wazee Magomeni Kota Omary Hemed amesema kuwa mkataba waliopewa umekuwa na utata wa kufanya kupteza haki yao na kukiuka makubaliano yaliyokuwepo hapo ya kuwa wapangaji na ununuzi wa nyumba za TBA Magomeni Kota.
Amesema muda waliopewa katika mkataba huo ni mdogo hivyo wanahitaji kuwepo na mabadiliano yenye afya kwa pande zote ya kufanyika kwa majadiliano hayo ndani ya siku 90 (miezi mitatu).
Hemed amesema kuwa wanaiomba serikali kwa wakazi 644 ambao wako katika nyumba kwani kwa kutumia mkataba mpya waliopeleka kutasababisha kupoteza haki zao.
Amesema marekebisho hayo yasipofanyiwa kazi watawasiliana na wakili kusudio la kuishitaki Serikali katika kipindi hicho kilichowekwa.
Aidha amesema kuwa mikataba mbalimbali imewekwa wa wakazi hao lakini kinachoibuka katika kipindi cha hivi karibuni ni kufanya mikataba hiyo haitambuliki kwa kila siku kuja na utaratibu wa nje na mikataba.
Hemed amesema rasimu ya mkataba tulioletewa unaipendelea TBA hivyo kusudi tuweze kupata au tuwe na uwanja sawa ni Mahakama kuu tu ndio inayoweza kutupa haki hiyo imefafanuliwa kwenye rasimu hiyo kipengele cha 12.
Nae mkazi wa Magomeni Kota na mjumbe wa kamati zote mbili Mkurumah Monjori amesema kuwa masuala yote ya wakazi wa kota yalifanyika kwa sheria kwa kuingiwa na mikataba baina ya pande zote mbili.
Amesema kuwa wamekutana na viongozi akiwemo Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni na Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam wamezungumza nao cha kushangaza baada ya muda wanakuja na mkataba ambao hawajakubaliana kuhusiana na Mpangaji Mnunuzi.
Amesema suala la mkataba ni suala la kisheria na haya ni maandishi yanayodumu hivyo tunahitaji umakini wa hali ya juu.Akarejea nukuu ya Katibu wa wezee mzee Omari.
Kifungu cha 12 kinatoa fursa ya kwenda Mahakama kuu.
Aidha amesema walichokifanya baada ya wakili kuwapa mrejesho kuwa muda waliopewa na Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni kuwa wawe wamifikia muafaka katika muda wa wiki mbili, Mwanasheria mkuu wa TBA ametoa jibu kuwa hawako tayari kubadili kipengele chochote.
Akiendelea kuelezea shauri hili Munjori alizidi kufafanua kuwa waliendelea na juhudi za kidiplomasia kwa kushirikiana na Mwenyekiti wa Mkoa CCM ambaye nae aliomba kukutana na uongozi wa juu wa TBA akiwa na kamati aliyoiunda mwenyewe kwenye mkutano mkuu maalum wa Magomeni Kota nazo ziligonga mwamba kwani siku tuliyokwenda Mtendaji mkuu wala aliyemkaimisha hawakuwepo licha ya kwamba waliomba kukutana nae na kufanya kupanga wenyewe bili ushirikishwaji
Monjori amesema lile azimio lililo sitishwa kwa ombi la Mwenyekiti CCM Mkoa utekelezaji wake ndio huu.
Hata hivyo walifatilia agizo la Mkuu wa Mkoa Dar es Salaam kutoa muda wa mwezi mmoja aliwajibu kuwa dhumuni la Mkuu wa Mkoa lilikuwa kufungua soko.
Taratibu za kisheria kufungua shauri Mahakama Kuu kama utekelezaji wa azimio la mkutano mkuu umeshafanyika na taarifa rasmi zimeshapelekwa kote kunakohusika ikiwemo TBA