Jeshi la Somalia laua magaidi 80 wa Al Shabab – Global Publishers




Vikosi vya usalama vya Somalia vimewaua zaidi ya magaidi 80 wa Al-Shabaab, wakiwemo vinara waandamizi wa kundi hilo, katika operesheni za wiki nzima dhidi ya kundi hilo lenye mafungamano na mtandao wa kigaidi al-Qaeda.

Kwa mujibu wa taarifa zilizotolewa jana Jumapili, operesheni hizo zilifanyika katika maeneo ya Shabelle ya Chini na ya Kati. Shirika la Kitaifa la Ujasusi na Usalama Somalia (NISA) limesema: “NISA, ikishirikiana na Jeshi la Kitaifa la Somalia, imefanya operesheni sita katika maeneo ya Shabelle ya Kati na ya Chini, na kuwaua zaidi ya Khawarij (waasi) 80, wakiwemo viongozi na wanamgambo.”

Operesheni hizo zimekuwa na ushindi mkubwa dhidi ya “Khawarij,” zikionyesha mafanikio katika kufutilia mbali mabaki ya ugaidi. Serikali ya Somalia hutumia neno “Khawarij” kuashiria kundi la kigaidi la Al-Shabaab

Wakati huo huo, Wizara ya Ulinzi ya Somalia, imemshukuru waziri wa muda mrefu wa ulinzi anayeondoka, Abdulkadir Mohamed Nur, ikisema chini ya uongozi wake, zaidi ya magaidi 5,000 wa Al-Shabaab wameuawa katika kampeni ya kupambana na ugaidi yenye mafanikio makubwa katika historia ya Somalia.

Somalia imekuwa ikisumbuliwa na ukosefu wa usalama kwa miaka mingi, huku vitisho vikuu vikitoka kwa makundi ya kigaidi ya Al-Shabaab na Daesh (ISIS).











Related Posts