By Ngilisho TvĀ
Watu thelathini wamefariki dunia katika mafuriko yaliyokumba Kinshasa, mji mkuu wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo.
Mvua kubwa iliyonyesha mwishoni mwa juma imeharibu makazi na miundo mbinu za mitaa ya mji huo.
Mto Ndijili unaopita katika mji huo wenye wakazi karibu milioni kumi na saba, ulivunja kingo zake Ijumaa usiku na kuathiri usafiri wa magari.
Mitaa kadhaa ya Kinshasa pia haina umeme na maji safi ya kutumia.
Zaidi ya nyumba 600 zilizozama ziko karibu na mji wa Masina, wilaya ya Abattoir, na Petro Kongo.
Mitumbwi na boti za mwendo kasi zinatumika kuokoa watu walioathirika na kuwahamisha waathiriwa hadi eneo salama.
“Kikao cha dharura kitafanyika ili kuamua jinsi ya kusaidia idadi ya watu,” alisema Naibu Mkuu wa Polisi Blaise Kilimbalimba, Kamanda wa Polisi wa Kinshasa.
Msimu wa mvua wa DRC kwa kawaida huanza Mwezi Novemba hadi Mei.