JK AWASILISHA UJUMBE WA RAIS SAMIA KWA RAIS MUSEVENI WA UGANDA LEO JIJINI KAMPALA

Pembenzoni mwa Mkutano wa Uongozi wa Afrika wa nane jijini Kampala Uganda leo, Mheshimiwa Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete, Rais Mstaafu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, akiwa kama mjumbe maalum, amewasilisha ujumbe maalum kwa Rais Yoweri Kaguta Museveni kutoka kwa Mheshimiwa Rais Samia Suluhu Hassan.
Rais Museveni alimshukuru kwa ziara na kumuomba amfikishie salamu zake kwa Mheshimiwa Rais Samia na watu wa Tanzania.

Related Posts