BOLT YAZINDUA HUDUMA YAKE KAHAMA,YAKUSUDIA KUBORESHA USAFIRI NA UCHUMI

 

*****

Kampuni ya usafiri wa mtandaoni Bolt, inayoongoza nchini Tanzania, imezindua rasmi huduma zake katika mji wa Kahama, hatua inayochukuliwa kuwa mafanikio makubwa katika juhudi zake za kuleta suluhisho la usafiri wa kisasa, wa kuaminika na nafuu kwa mikoa mingi zaidi nchini.

Uzinduzi huo ni sehemu ya mkakati mpana wa Bolt wa kuimarisha usafiri mijini na kuwa wezesha jamii za nje ya miji mikuu. Uwepo wa Bolt Kahama unatarajiwa kubadilisha namna ambavyo wakazi, wafanyabiashara wadogo na wasafiri wa kila siku wanavyohama kutoka eneo moja kwenda jingine katika mji huu wenye shughuli nyingi za biashara na uchimbaji madini.

Kwa mujibu wa taarifa ya mwaka 2023 kutoka UN-Habitat, miji ya Tanzania ni miongoni mwa miji yenye idadi kubwa ya watu barani Afrika, hasa kutokana na uhamiaji kutoka vijijini kwenda mijini.

 “Utafiti wa mwaka 2015 ulibaini kuwa asilimia 61.4 ya wakazi wa mijini walihamia kutoka vijijini, huku asilimia 38.6 walizaliwa mijini,” inaeleza ripoti hiyo, ikisisitiza kuwa maendeleo ya miundombinu, umeme na fursa za ajira ndizo huvutia watu kuhamia mijini.

Dimmy Kanyankole, Meneja Mkuu wa Bolt Tanzania na Kenya, amesema:”Mji wa Kahama sio tu miongoni mwa maeneo ya mijini katika mkoa wa Shinyanga, bali pia ni eneo la kimkakati lenye shughuli nyingi za kiuchumi na uwezekano mkubwa wa ukuaji. Kuingia kwetu katika eneo hili ni sehemu ya dira ya Bolt ya kuchangia ujenzi wa miji rafiki kwa watu.

 Urahisi wa usafiri unaoshuhudiwa Dar es Salaam, Arusha na Mwanza sasa unaweza kuwa sehemu ya maisha ya kila siku ya wakazi wa Kahama.”

Huduma ya Bolt inatarajiwa kuongeza ajira kwa vijana, kwa kuwapa nafasi ya kujiandikisha kama madereva washirika.

 Jukwaa hili pia litachochea mwendo wa wateja, jambo ambalo litafungua fursa kwa wafanyabiashara wa eneo hilo, watoa huduma na taasisi nyingine. 

Kwa mujibu wa Halmashauri ya Manispaa ya Kahama, asilimia 40 ya wakazi wa mji huo hufanya shughuli zao katikati ya eneo la biashara.

Kwa kuwa mji wa Kahama una kasi ya ukuaji wa asilimia 8.7 kwa mwaka, ikilinganishwa na asilimia 3.2 ya ukuaji wa mkoa mzima wa Shinyanga, uzinduzi wa Bolt Kahama ni sehemu ya ushirikiano kati ya sekta binafsi na serikali katika kupunguza changamoto za usafiri, kutoa huduma salama zinazofuata kanuni za usafiri, na kuchangia katika kidigitali cha sekta ya usafiri wa umma — ikiwa ni sehemu ya malengo ya taifa ya ujumuishaji wa kifedha na maendeleo yanayoendeshwa na teknolojia.

Related Posts