INAELEZWA kuwa upo uwezekano mkubwa wa kiungo mshambuliaji wa Yanga, Stephene Aziz Ki wa kuondoka mwishoni mwa msimu huu.
Kwa mujibu wa Chanzo cha Habari kutoka Yanga, Uongozi upo katika mipango ya kumfuata Feisal Salum ‘Fei Toto’ ili arejee kikosini kumrithi Aziz Ki.
Klabu ya Wydad Casablanca ya nchini Morocco ndiyo inatajwa kumsajili kiungo huyo ambaye tayari amewaambia Yanga anataka kwenda kucheza Fifa Club World Cup 2025 inayotarajiwa kufanyika Juni 14, Marekani.