****
Naibu waziri wa Nishati Dotto mashaka Biteko amesema serikali inatakiwa kujipanga katika kujenga miradi ya umeme kuanzia sasa ilikuepuka madhara ya kukosa umeme kwa miaka ijayo.
Dkt Biteko ameyazungumza haya leo 9 Aprili 2025 jijini Dodoma ,wakati wa uzindunzi wa Taarifa za maendeleo ya sekta ya Nishati kwa mwaka 2023_2024 .
Aidha megawait 8059 zitahitajika kufikia 2030 ambapo matumizi ya nishati ya umeme yataongezeka kutokana na shughuli nyingi za kiuchumi zinazofanywa na wananchi .
Vilevile Biteko ameitaka Mamlaka ya udhibiti wa huduma za Nishati na maji (Ewura )kuendelea kusimamia sekta ya mafuta ,sekta ndogo ya umeme na sekta ndogo ya gas asilia ili kuendelea kufanya kazi kwa weledi.
Mwisho Naibu waziri amesema mabadiliko tabia nchi yamekuwa yakichangia katika kuhalibu miundombinu inapelekea kuwa na marekebisho ya miundombinu ya mara kwa mara .