MUHAS KUTOA ELIMU NA WATAALAMU WA KUKABILI USONJI

Mkurugenzi wa Magonjwa yasiyoambukiza, Afya na Akili wa Wizara ya Afya, Dk Omary Ubugoyu akizungumza jambo katika Kongamano la Kitafiti linalozungumzia ugonjwa wa usonji lililofanyika katika Chuo Kikuu cha Afya na Sayansi Shirikishi Muhimbili (MUHAS) leo April 9, 2025, Dar es Salaam

.…………..

Chuo Kikuu cha Afya na Sayansi Shirikishi Muhimbili (MUHAS) kimesema  kimejipanga kuendelea kuelimisha jamii kuhusu ugonjwa wa usonji pamoja na kuzalisha wataalamu wa shahada ya awali ya mazoezi ya viungo (Physiotherapia), kufundisha matamshi (speech therapy), kusaidia wenye matatizo ya viungo ili kuhakikisha wanatokomeza ugonjwa huo.

Akizungumza katika Kongamano la Kitafiti linalozungumzia  ugonjwa wa usonji lililofanyika MUHAS leo April 9, 2025, Dar es Salaam, Mkurugenzi wa Magonjwa yasiyoambukiza, afya na Akili wa Wizara ya Afya,  Dkt. Omary Ubugoyu, amesema kuwa  kwa sasa wanahakikisha wanafanya ugunduzi wa mapema hospitalini na shuleni kutambua watoto wenye usonji.

Dkt. Ubugoyu amesema kuwa wapo watoto kwenye usonji ambao hawapelekwi hospitalini, hivyo kwa kupitia shule watawagundua mapema na kuwapatiwa tiba stahiki kwa wakati.

Amesema kuwa wanaongeza idadi ya wahudumu wa afya katika hospitali za ngazi za rufaa za mikoa waweze kuwatambua wagonjwa, huku akieleza  Mkoa wa Dar es Salaam kuna shule za awali  100 na walimu 4,000 ambao watafundishwa namna ya kumgundua mtoto mwenye usonji.

“Serikali ina mkakati wa kuongeza watoa huduma wa matibabu bingwa ambao watakuwa wataalamu wa tiba ya viungo,  kazi,  saikolojia na matamshi,” amesema Dkt. Ubugoyu.

Amesisitiza kuwa 2023 walianza kutoa mafunzo ya  mwaka ambapo wamepata wataalamu 50 wa awamu ya kwanza ambao wanatarajia kuanza kutoa huduma.

Makamu Mkuu wa MUHAS, Profesa Appolinary Kamuhabwa amesema kuwa wameanzisha shahada ya awali ya mazoezi ya viungo (Physiotherapia), shahada ya kufundisha matamshi (speech therapy) na shahada ya kusaidia wenye matatizo ya viungo.

Amesema kwa kuwa jukumu lao ni kufundisha watoa huduma za afya na kufanya tafiti, ili kuhakikisha wanazalisha zaidi wataalamu watakaosaidia watoto wenye usonji kukabiliana na changamoto zao.

“Mapendekezo tunayotoa ni kuwasaidia watunga sera kufanya maboresho, wazazi na jamii namna ya kuishi nao na kuacha kuwanyanyapaa,” amesema Profesa Kamuhabwa.

Mkuu wa Idara ya Utafiti MUHAS, Profesa Bruno Sunguya, amesema  mwezi Aprili  kwa ajili ya kuelimisha umma  kuhusu usonji na kwamba tatizo hilo limekuwa likiongezeka kutokana na kuwepo wataalamu wa kuutambua.

“Dalili zake mtoto au mkubwa kushindwa kuwasiliana, kujitenga na wenzake na zikigundulika mapema, mtoto mwenye usonji sio mlemavu na kwamba anaweza kubadilika mapema akipatiwa matibabu mapema,” amesema Profesa Bruno Sunguya.

Naibu Makamu Mkuu MUHAS, Idara ya Utafiti na Ushauri wa Kitaalamu Profesa Bruno Sunguya, amesema kuwa mwezi wa nne kwa ajili ya kutoa elimu kwa umma kuhusu masuala ya usonji.

Amesema kuwa tatizo la usonji limekuwa likiongezeka, kumetokana na ungezeko la wataalamu ambao wanauwezo wa kutambua ugonjwa huo.

Profesa Sunguya, amesema kuwa dalili za ugonjwa wa usonji ni pamoja na mtoto mdogo kushindwa kuongea pamoja na kukosa maendeleo ya ukuaji kama inavyotakiwa.“Wakati mwengine mtoto anakaa peke yake akifanya shughuli zake, kushindwa kuwasiliana.

Akizungumza wakati wa kongamano la 15 la kisayansi lililofanyika jana katika Chuo Kikuu cha Afya na Sayansi Shirikishi Muhimbili (MUHAS), Daktari Bigwa wa Watoto, Profesa Karimu Manji, amesema kuwa wazazi wengi wamekuwa na utaratibu wa kuwaachia mtoto jambo ambalo sio rafiki.

“Screen time  kwa watoto chini  ya miaka mitano ni hatari sana, mzazi jaribu kufuatilia,  katuni kwa kumuelekeza mtoto kila kinachofanywa na namna kinavyotamkwa, kuwe na ufundishaji na sio kumtelekezea mtoto aangalie mwenyewe ili kumnyamazisha si sahihi,” amesema Profesa Manji.

Profesa Manji  amesema kuwa vyakula vya kopo, dawa za kuua wadudu na za kufanya nyumba inukie, zinapaswa kutumiwa kwa uangalifu kwani zina athari kwenye ubongo wa mtoto.

“Tusiwanyanyapae watoto hawa na tiba yao ni kuwagundua mapema na kuanza kuwapatia tiba ya matamshi na viungo ambazo gharama yake ni kubwa kwa siku ni 100,000 na kwa vile ni endelevu, wazazi wanafilisika tunahitaji mkakati wa makusudi katika sera zetu,” amesema Profesa Manji.

Amesema kuwa  mtu mwenye usonji awapo kazini hulalamikiwa kwa kutochangamana na watu, kuwa mtaratibu kupitiliza na kufanya mambo yake binafsi.

“Wazazi msiwe wanyonge, watoto hawajarogwa, wanaweza kubadilika tabia na kuwa wataalamu bingwa au wenye kuaminika katika jamii,”amesema.

Makamu Mkuu wa MUHAS, Profesa Appolinary Kamuhabwa Profesa Appolinary akizungumza jambo katika Kongamano la Kitafiti linalozungumzia ugonjwa wa usonji lililofanyika katika Chuo Kikuu cha Afya na Sayansi Shirikishi Muhimbili (MUHAS) leo April 9, 2025, Dar es Salaam.

Mkuu wa Idara ya Utafiti MUHAS, Profesa Bruno Sunguya akizungumza jambo katika Kongamano la Kitafiti linalozungumzia ugonjwa wa usonji lililofanyika katika Chuo Kikuu cha Afya na Sayansi Shirikishi Muhimbili (MUHAS) leo April 9, 2025, Dar es Salaam.

  Daktari Bigwa wa Watoto, Profesa Karimu Manji akizungumza jambo katika Kongamano la Kitafiti linalozungumzia ugonjwa wa usonji lililofanyika katika Chuo Kikuu cha Afya na Sayansi Shirikishi Muhimbili (MUHAS) leo April 9, 2025, Dar es Salaam.

     

Related Posts