Shirika la Umeme Tanzania(TANESCO) linawajulisha wateja wake wa mkoa wa Songwe, Njombe, Mbeya, Ruvuma na Wilaya ya Masasi kutakuwa na matengenezo katika kituo cha kupoza umeme cha Makambako. Kutokana na matengenezo hayo baadhi ya wateja watakosa huduma kesho Jumamosi kuanzia saa mbuli asubuhi mpaka saa kumi na moja jioni.