TAWIFA YAJA NA KAMPENI YA MTI PESA MASHULENI.

Na Janeth Raphael MichuziTv -Dodoma

Hamasa yatolewa kwa Wadau wa Maendeleo ikiwemo Sekta ya Kilimo,Sekta ya Misitu na Mazingira kuungana Rais Dkt Samia kupitia Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Dodoma kwa kupanda miti katika maeneo mbalimbali kama vile Majunbani, barabara,Taasisi na sehemu zingine za kimkakati zilizowekwa maalum ya kwaajili kupandwa miti.

Wito huo umetolewa na Katibu Tawala Mkoa wa Dodoma Bwana Kaspar Mmuya leo Jijini Dodoma Machi 11,2025 katika zoezi la upandaji miti lililofanyika katika maeneo ya wazi ya shule ya msingi Mtumba lilioratibiwa na Chama cha Wanawake kwenye Sekta ya Fedha(TAWIFA) ambalo limeenda sambamba na Uzinduzi club za Fedha Mashuleni inayolenga kuwajenga uelewa wa nidhamu ya fedha watoto kuanzia katika utoto wao.

“Natoa hamasa kwa Wadau wote wa Maendeleo hususan sekta ya Kilimo,Sekta ya Misitu na Sekta ya Mazingira,tafadhali ungana na Rais kupitia ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Dodoma katika kupanda miti kwenye Taasisi,kwenye nyumba tunazokaa,kwenye barabara na sehemu zingine zote za kimkakati zilizotengwa maalum kwa kupanda miti”.

Aidha Katibu Tawala huyo amesema lengo la kupanda miti hiyo ya Matunda mashuleni ni pamoja na kuwafundisha watoto kuwa chanzo cha mapato kinaweza kupatikana hata kwa kupanda miti hasa miti ya matunda.

“Kwa Wastani kipato cha mtu mmoja mmoja Dodoma hakizidi milioni 2 kwa mwaka, kwahiyo tukasema kwa kupanda miti ya matunda tunategemea kiwe ni chanzo kikubwa cha familia na mtu mmoja mmoja kukuza kipato,kwahiyo tumeanza na shule tano ikiwemo hii ya Mtumba kwa kupanda miti 500 lakini kwa zote 5 tutapanda miti 2000 lengo likiwa ni kufundisha watoto kuwa chanzo cha mapato kinaweza kupatikana hata kwa kupanda miti hususan ya Matunda”.

Naye Rais wa Chama cha Wanawake kwenye Sekta ya Fedha (TAWIFA) Bi. Fikira Ntomola amesema kuwa wao wanataka kuonesha kuwa kupanda miti sio kwaajili ya kutunza Mazingira tu bali hata katika kuchochea uchumi wa Nchi kwa kuhamasisha kupanda miti ya Matunda kwani ina faida mbeleni kama itatunzwa vyema kama wao wanavyofanya katika Kampeni yao.

“Tawifa inazundua Kampeni kubwa inayoitwa mti pesa na imekuja na Kampeni hii kwaajili ya kusukuma zaidi ajenda ya kukijanisha Dodoma lakini kukabailiana na mabadiliko ya tabia ya nchi na hali ya hewa kwa ujmla tukianza na Mkoa wa Dodoma ambapo pia tunataka kuonesha kuwa kupanda miti sio kwaajili ya kutunza Mazingira tu lakini pia inachochea uchumi wa nchi yetu “.

Aidha ameongeza kuwa Kampeni hii ni kumsapoti Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt Samia Suluhu Hassan kwani amekuwa ni kiongozi na mfano wa kuigwa katika jukumu la upandaji miti na kuhakikisha nchi ya Tanzania inakuwa ni nchi ya kijani ndomana wameamua kuungana nae.

Pia akielezea uhusiano uliopo kati ya fedha na Utunzaji wa Mazingira amesema kuwa wao zoezi wanalofanya ni kupanda miti ya matunda ambayo haimpi mtu kivuli au kutunza Mazingira na kuwa na mvua za kutosha tu bali mti utakapokua na kuleta matunda ndipo fedha inapoweza kupatikana kupitia uuzaji wa matunda hayo.

Kwa upande wake Mkuu wa Shule ya Msingi Mtumba Bwana Kepha Kitutu ameahidi kusimamia na kutunza miti hiyo mpaka itakapokua na kusema kuwa upatikanaji wa miti hii utasaidia kwa kiwango kikubwa sana kwanza katika kutunza na kuimarisha mazingira lakini pia uwepo wa fursa mbeleni iatakapotunzwa vizuri.

Uzinduzi huu wa upandaji miti na Club za fedha Mashuleni utafuatiwa na Utoaji wa elimu ya fedha kwa Wanawake wajasiriamali pamoja Mkutano wa mwaka wa Chama Cha Wanawake kwenye Sekta ya Fedha .




Related Posts