Familia ya kijana Raphael Majembe ya Tabata Shule jijini Dar es Salaam, imegoma kuchukua mwili wa kijana wao mochwari kwa ajili ya kwenda kuuzika wakidai wanataka uchunguzi wa kina ufanyike kwani ndugu yao amefariki dunia akiwa kwenye mikono ya Jeshi la Polisi.
Mmoja kati ya wanafamilia ameeleza namna walivyofuatwa na Jeshi la Polisi lakini mtuhumiwa walimkosa lakini walimbeba yeye.