TADED:HAKUNA CHAMA CHA KUZUIA UCHAGUZI MKUU USIFANYIKE

********

Na Mwandishi Wetu.

Taasisi ya Demokrasia na Maendeleo Tanzania  (TADED) imesema kuwa hakuna chama au taasisi
ya kufanya kuzuia uchaguazi Mkuu ambao hufanyika kila baada ya miaka mitano.

Akizungumza jijini Dar es Salaam Mwenyekiti wa
TADED Chalila Kibuda amesema kuwa  kwa
mujubu wa Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupiga kura ni haki ya
watanzania hivyo hawezi  chama au Taasisi
kuwazuia wananchi wasipige kura.

Amesema TADED katika kipindi cha kuelekea
uchaguzi kitahakikisha kinahamasisha wananchi kushiriki katika mchakato wa
uchaguzi mkuu katika kusikiliza mikutano ya kampeni  kutoka kwa 
wagombea pamoja na kushiriki kupiga kura.

Amesema katika kampeni hizo kwa wagombea kunadi
sera za vyama vyao na sio kukashifiana ambapo hizo kashfa sio kipaumbele kwa
wananchi wanaotaka maendeleo kwa viongozi wataowachagua.

“Uchaguzi 
huu ni haki ya kila mwananchi kushiriki katika kuchagua viongozi
wataodumu kwa kipindi cha miaka mitano kwa mujibu wa Katiba  ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania”.amesema

Aidha amesema suala la chaguzi Mkuu  kwa katiba hii hakuna chombo chochote
kinachoweza kuzuia kutofanyika uchaguzi ambapo hata chama kilichopo madarakani
hakiwezi kufanya hivyo.

Hata hivyo katika maandalizi hayo yamefanyika
vizuri ikiwemo wananchi kujiandikisha katika daftari la wapiga kura nchi nzima.

Kibuda amesema chama  fulani kinasema No Reform.No election ni
jambo ambalo haiwezekani kuleta katikati ya zoezi hilo kuanza.

 

Hata hivyo tangu tumefanya uchaguzi 2020 katika
kipindi hicho walikuwa nafasi ya kufanya juu ya kuliendea jambo la uchaguzi na
serikali  ikachukua hatua.

 

Hata hivyo Serikali ya awamu ya sita chini
Dkt.Samia Suluhu Hassan katika kuweka utulivu wa Siasa amefanya mambo pamoja na
kuwa na maridhiano ya kuruhusu mikutano kufanyika ambapo vyama vinaendelea
kufanya mikutano bila vikwazo.

Aidha katika mazingira tulionayo nchi iko tulivu
kabisa kila mwananchi anaendelea kufanya maisha yake hii inaonyeesha amani
ambapo  Rais na vyombo vyake kuendelea
kuhudimia wananchi wake.

 

Amesema nchi iko salama  na kufanya mataifa mbalimbali kuwekeza kwa
kigezo kuwa na siasa salama (political Stability).

 

Katika maendeleo 
nchi chini Rais Dkt.Samia Suluhu Hassan 
imeendelea kutekeleza miradi yote ikiwemo bwawa la umeme la Nyerere
ambapo hadi sasa umekamilika ,huku ujenzi wa Reli ya Kisasa SGR unaendelea
kuanzia Dodoma hadi Mwanza.

 

Katika sekta ya Utalii nchi imekuwa na watalii
ambao wanaongezeka  hiyo  inatokana na serikali ya Dkt.Samia Suluhu
Hassan kutengeneza filam ya Royal Tour kwa ajili kutangaza utalii

 

Amesema nchi imeendelea kujiimarisha katika
mahusiano ya kimataifa kwa Rais kufanya ziara ambapo ndio matokeo yanayooneka
katika uwekezaji nchini.

Katika mikakati iliyojiwekekea Taasisi ni
pamoja  na kufanya makongamano nchi nzima
kwa kushirisha wasanii mbalimbali ambapo mazungumzo yao yanaendelea kufanyika
na hatuwezi kuyatoa kwenye vyombo vya habari pamoja na kukutana viongozi wa wa
dini katika katika kilele cha kampeni viongozi hao kutoa ujumbe kuhusiana na
uchaguzi.

Related Posts