Rekodi mbili zambeba Clara Saudia

ZIMESALIA mechi mbili kumalizika kwa Ligi ya Wanawake Saudia, lakini Mtanzania pekee, Clara Luvanga anayekipiga (Al Nassr) ameweka rekodi mbili msimu huu akiwa na kikosi hicho.

Nyota huyo wa timu ya taifa ya Wanawake, Twiga Stars huu ni msimu wa pili tangu alipojiunga na timu hiyo akitokea Dux Lugrono ya Hispania alipocheza miezi mitatu.

Al Nassr imebeba ubingwa msimu huu kabla ya kumaliza mechi mbili ikukusanya pointi 48 katika mechi 16 ambazo haziwezi kufikiwa na timu yoyote.

Rekodi ya kwanza aliyoweka straika huyo wa zamani wa Yanga Princess kufunga mabao 14 na asisti saba akiwa ndio kinara wa ufungaji wa Al Nassr.

Msimu wa kwanza katika mechi 18 alifunga mabao 11 na asisti sita akimaliza nafasi ya tatu kwenye tuzo za wafungaji bora ambayo aliibuka nayo Ibtissam Jraidi wa Al Ahli.

Rekodi ya pili kutetea ubingwa wa Al Nassr bila kupoteza mchezo wowote ukiwa wa pili kwa Clara na wa tatu mfululizo kwa kwa klabu hiyo ilipobeba kuanzia 2022/23.

Related Posts