****
Wachungaji wa Makanisa ya Pentekoste Jijini Dar es Salaam wamesema, wameichagua siku ya June 21 mwaka huu kuwa ya kuuombea uchaguzi mkuu wa urais, wabunge na madiwani ili uwe wa haki na amani.
Wakizungumza Jijini Dar es Salaam katika kikao cha maandalizi kuelekea maombi hayo ya kitaifa yatakayohusisha mikoa 26 nchini, Mwenyekiti wa Makanisa Pentekoste Mkoa wa Dar es Salaam Emanuel Mwasota amesema suala la maombi halina mjadala, hivyo kujilinda na yanayotokea nchi jirani ni jambo la kutiliwa mkazo.
Kwa upande wake Mwenyekiti wa Kamati ya Maandalizi kuhusiana na maombi hayo Mkurugenzi wa Kampuni ya Msama Promotion Alex Msama amesema mbali ya wachungaji na viongozi mbalimbali wa dini kushiriki pia tamasha hilo litawahusisha waimbaji wakubwa wa muziki wa injili kutoka ndani na nje ya nchi.
Baadhi ya wachungaji washiriki akiwemo Mchungaji Rose David wa Kanisa la Saa ya Uwokovu ni Sasa lililopo Viwege amesema, amani na umoja uliopo unatakiwa ulindwe kwa maombi kutoka kwa wananchi na viongozi wa dini.