WADAU WA UNUNUZI WAASWA KUZINGATIA MAADILI KAZINI

Katibu Mtendaji wa PPAA, Bw. James Sando akiongea na wazabuni na wadau wa ununuzi wa Umma kutoka taasisi za Serikali (hawapo pichani) kwa Kanda ya Kaskazini mwishoni mwa wiki jijini Arusha

*****

Na Mwandishi Wetu, Arusha.

Wadau wa Ununuzi waaswa kuzingatia maadili na elimu katika Ununuzi wa Umma ili kuiwezesha Serikali kupata thamani halisi ya fedha. 

Wito huo umetolewa mwishoni mwa wiki na Katibu Mtendaji wa Mamlaka ya Rufani ya Zabuni za Umma (PPAA), Bw. James Sando alipokuwa akifunga mafunzo ya siku mbili kuhusu matumizi ya Moduli ya kuwasilisha na kushughulikia malalamiko na rufaa kwa njia ya kielektroniki katika mfumo (NeST) kwa wazabuni na wadau wa ununuzi wa Umma kutoka taasisi za Serikali kwa Kanda ya Kaskazini yaliyofanyika jijini Arusha.

Bw. Sando amesema kuwa baadhi ya kesi zinazowasilishwa PPAA kwa asilimia kubwa zinakuwa zimesababishwa na ukiukwaji wa maadili. 

“Kama wadau katika sekta ya ununuzi wa umma ni muhimu sana kuzingatia maadili kwa sababu ndiyo itakayoipatia serikali thamani halisi ya fedha na heshima, sote tunajua mifumo ya ununuzi ipo lakini inaongozwa na binadamu kama hawana maadili mifumo haina maana,” alisema Bw. Sando

Bw. Sando aliongeza kuwa unaweza kutengeneza sheria nzuri sana lakini kama watu hawataamua kuwa watiifu wa sheria hiyo kutakuwa na uvuinjifu mkubwa wa sheria katika nchini hiyo.

“……vivyo hivyo hata sisi tukikosa maadili katika sekta ya ununuzi wa umma tutakuwa na kesi nyingi sana……kutakuwa na upotevu wa fedha za umma,” aliongeza Bw. Sando 

Kadhalika, Bw. Sando amewataka washiriki walipota fursa ya kuhudhuria mfunzo hayo kwa Kanda ya Kaskazini kuwaelimisha wadau wengine kuhusu matumizi ya moduli ya kuwasilisha na kushughulikia malalamiko na rufaa kwa njia ya kielektroniki (Complaint and Appeal Management Module) katika Mfumo wa Kielektroniki wa Ununuzi wa Umma (NeST).

Naye mmoja wa wadau wa ununuzi wa umma aliyeshiriki mafunzo hayo Bi. Rachel Werema aliipongeza PPAA kwa kuandaa mafunzo hayo ya siku mbili kwani yamewasaidia kufahamu namna ya kuwasilisha malalamiko na rufaa zitokanazo na michakato ya ununuzi kwa wakati kupitia moduli iliyopo katika mfumo wa NeST.

Mafunzo hayo ya siku mbili kwa Kanda ya Kaskazini yelifanyika jijini Arusha kuanzia tarehe 10 – 11 Aprili, 2025 yalihudhuriwa na washiriki 240 kutoka mikoa ya Arusha, Manyara, Kilimanjaro na Tanga. 

Awamu ya kwanza ya mafunzo kikanda yalifanyika Kanda ya Ziwa kwa siku tatu ambapo yalijumuisha washiriki zaidi ya 580 mkoani Mwanza kuanzia tarehe 4 – 6 Februari, 2025 yakijumuisha mikoa ya Mwanza, Geita, Mara, Kagera, Simiyu na Shinyanga.  

Katibu Mtendaji wa PPAA, Bw. James Sando akiongea na wazabuni na wadau wa ununuzi wa Umma kutoka taasisi za Serikali kwa Kanda ya Kaskazini mwishoni mwa wiki jijini Arusha

Meneja wa Usimamizi wa Rufaa na Huduma za Sheria PPAA, Bi. Florida Mapunda akiwasilisha mada kuhusu matumizi ya moduli ya kuwasilisha na kushughulikia malalamiko na rufaa kwa njia ya kielektroniki katika mfumo wa NeST kwa wazabuni na wadau wa ununuzi wa Umma kutoka taasisi za Serikali kwa Kanda ya Kaskazini mwishoni mwa wiki jijini Arusha

Mmoja kati ya washiriki wa mafunzo ya moduli ya kuwasilisha na kushughulikia malalamiko na rufaa kwa njia ya kielektroniki katika mfumo wa NeST akifafanua jambo wakati wa mafunzo yaliyofanyika mwisho wa wiki jijini Arusha 

Sehemu ya washiriki wa mafunzo ya moduli ya kuwasilisha na kushughulikia malalamiko na rufaa kwa njia ya kielektroniki katika mfumo wa NeST akifafanua jambo wakati wa mafunzo yaliyofanyika mwisho wa wiki jijini Arusha

Mwisho………

 

Related Posts