WANACHAMA 50 ACT Wazalendo LINDI WATIMUKIA CCM.

Zaidi ya wanachama 50 kutoka katika chama cha ACT Wazalendo wamejiunga na chama Cha mapinduzi ( CCM)

Wanachama hao wakiongozwa na aliyewahi kuwa diwani na mwenyekiti kupitia tiketi ya ACT Wazalendo, Said Kitunguli wamepokelewa na Katibu wa NEC, Itikadi, Uenezi na Mafunzo wa CCM, CPA Amos Makalla wakati akizungumza na wananchi kwenye mkutano wa hadhara Wilaya ya Lindi Mjini mkoani Lindi.

Awali, Makalla alikuwa akitambulisha wageni alioambatana nao hususani walio hamia kutoka katika vyama vya upinzani ili kutoa salamu zao kwa wananchi.

Miongoni wa walioambatana na Makalla katika msafara huo ni aliyewahi kuwa Mbunge wa Iringa na Mjumbe wa Halmashauri Kuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Mchungaji Peter Msigwa.

Pia aliambatana na Aliyewahi kuwa Mkuu wa Mawasiliano wa chama cha Wananchi (CUF), Abdul Kambaya akifuatiwa na Rashid Sepanga ambaye alihamia CCM Novemba, mwaka jana na kusema kuwa wanachama hao wapya walikuwa ni zawadi kwa CCM.

Aidha, akizungumza kwa upande wake Kitunguli alisema kuwa alikuwa mwanachama wa CCM mwaka 2008 alihama na kuhamia CUF akieleza utekelezaji wa Ilani ya CCM chini ya uongozi wa Rais Samia Suluhu Hassan ndo sababu kubwa ya kuwamfanya ahamie CCM.

“Mimi nilikuwa CCM 2008 nikatoka nikaenda kuusoma upinzani kitu kikubwa ambacho ndugu zangu mliobaki huko sijui mnabakia kwa lipi mimi nilikuwa diwani na nikawa mwenyekiti wa mtaa vyote sidhani uliko nje ulikuwa unabakisha nini,” amesema Kitunguli.

Ameongeza kuwa akiwa upinzani kitu walichojifunza ni ukaidi na vurugu lakini sio kufanya mambo yenye manufaa kwa wananchi.



Related Posts