Refa raia wa DR Congo kuamua Simba, Stellenbosch CAFCC

Refa mzoefu Jean Jacques Ndala kutoka DR Congo ndiye amepangwa kuchezesha mechi ya kwanza nusu fainali ya Kombe la Shirikisho Afrika baina ya Simba na Stellenbosch ya Afrika Kusini kwenye Uwanja wa New Amaan Complex, Aprili 20 mwaka huu.

Ngambo mwenye umri wa miaka 37, amewahi kuichezesha Simba katika mechi nne tofauti za kimataifa ambapo imeshinda mbili, imetoka sare moja na kupoteza moja.

Mechi ya kwanza kwa Ngambo kuichezesha Simba ilikuwa ni ya hatua ya makundi ya Ligi ya Mabingwa Afrika msimu wa 2018/2019 ambao ilipoteza kwa mabao 2-0 mbele ya JS Saoura ya Algeria ugenini.

Refa huyo akachezesha mechi ya raundi ya kwanza ya ligi ya mabingwa Afrika msimu wa 2021/2022 ambayo Simba ilipata ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya Jwaneng Galaxy ya Botswana.

Msimu huohuo, Ndala alichezesha mechi ya nyumbani ya hatua ya makundi ya Kombe la Shirikisho Afrika ambayo Simba ilipata ushindi wa bao 1-0 dhidi ya RS Berkane ya Morocco.

Mchezo wa mwisho kwa Ndala kuichezesha Simba ulikuwa ni ugenini wa mashindano ya African Football League ambao Simba ililazimisha sare ya bao 1-1 dhidi ya Al Ahly ya Misri.

Refa huyo amechezesha idadi ya michezo 81 ya kimataifa na ametoa zaidi ya kadi 200 na kati ya hizo, nyekundu ni sita.

Related Posts