TAHARUKI YATANDA MERERANI WANAAPOLO WAHOFIWA KUFIA MIGODINI ,FAMILIA ZAWEKA KAMBI LANGO KUU LA KUINGILIA KUTAKA NDUGU ZAO,MIGODI KADHAA YATAJWA KUHUSIKA!

 Na Joseph Ngilisho MERERANI 


WACHIMBAJI watatu wadogo wa madini Tanzanite (Wanaapolo) Mererani ,wanahofiwa kufa kwa kufukiwa ndani ya migodi ya madini hayo katika mji mdogo wa  Mererani wilayani Simanjiro Mkoani Manyara,baada ya wazazi wao kutowaona kwa siku kadhaa na kuandamana katika lango kuu la Mererani wakitaka kupata taarifa za ndugu zao.

Taarifa za kutoonekana kwa wanaapolo hao zilianza kuzagaa katika viunga vya migodi hiyo ya Mererani kuanza aprili 12 wiki iliyopita huku ndugu wa jamaa hao wakionekana kulizonga lango kuu la Mererani wakitaka kujua ndugu zao wako wapi.

Katika kikao kilichoketi jumamosi na leo jumatatu katika  ofisi ya Afisa mfawidhi wa Madini Mererani RMO,hoja kubwa ni namna ya kupata taarifa za wachimbaji hao ambao hawakuwa sehemu ya wameajiriwa katika migodi inayohofiwa kufia ndani.

Mkuu wa wilaya ya Simanjiro,Fakii Raphael Lulandala amethibitisha kuwepo kwa taarifa za kupotea kwa wachimbaji hao na kudai kwamba jitihada za kuwasaka katika migodi kadhaa inayohofiwa kufanya kazi kwa watu hao  zimefanyika ila hadi sasa bado hawajaonekana tangu taarifa hizo ziwafikie aprili 12,Mwaka huu .

“Tupo katika zoezi la kuwasaka watu hao ,ambao zipo hisia kwamba wamefia migodini ,hadi sasa hatujapata ukweli hadi wapatikane ,ipo migodi mikubwa wanayohofiwa watu hao kuingia ndani na upekuzi umefanyika na unaendelea”

Mkuu huyu wa wilaya ambaye hakuwa tayari kuweka wazi migodi hiyo ,alisema kuwa bado vyombo vya dola vinaendelea uchunguzi wa jambo hilo na taarifa zaidi zitatolewa baada ya kukamilisha uchunguzi.

Kutokana na taarifa hizo kuzagaa  katika mgodi huo wa Mererani,hofu imetanda katika machimbo hayo huku baadhi ya migodi inayohofiwa watu hao kuinga kinyemela ikitajwa na kuitaka serikali kuongeza uchunguzi ili kuwapata watu hao.

End….

Related Posts