Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa Leo Aprili 14, 2025 atafungua mkutano wa 15 wa Taasisi ya Maboresho katika Mamlaka za Serikali za Mitaa (TOA) unaofanyika katika ukumbi wa Jiji, uliopo kwenye Mji wa Serikali, Mtumba jijini Dodoma
Mkutano huo unalenga kubadilishana uzoefu na kuwajengea uwezo wanachama wa TOA ili kuwawezesha kuleta mabadiliko chanya ya mwelekeo wa utendaji wa kila siku na kuchagiza maboresho katika Serikali za Mitaa.
Moja ya jukumu la TOA ni kuishauri Serikali katika masuala mbalimbali yanayohusu ustawi wa Mamlaka za Serikali za Mitaa.
Mkutano huo umehudhuriwa na Makatibu Tawala wa Mikoa na Wakurugenzi wa Mamlaka za Serikali za Mitaa.