Waziri Mkuu, Mhe. Kassim Majaliwa akitoa hoja ya kuhitimisha mjadala wa bajeti ya Ofisi ya Waziri Mkuu, Taasisi zake na Mfuko wa Bunge kwa mwaka wa fedha 2025/2026 wakati wa Kikao cha Sita cha Mkutano wa 19 wa Bunge la 12, leo tarehe 15 Aprili, 2025 Bungeni Dodoma.
Waziri Mkuu, Mhe. Kassim Majaliwa akiwapongeza watendaji wa Ofisi yake mara baada ya bunge kupitisha bajeti ya Ofisi ya Waziri Mkuu, Taasisi zake na Mfuko wa Bunge kwa mwaka wa Fedha 2025/2026 wakati wa bunge linaloendelea jijini Dodoma.
Waziri Mkuu, Mhe. Kassim Majaliwa akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya Watumishi wa Ofisi yake mara baada ya bunge kupitisha bajeti ya Ofisi ya Waziri Mkuu, Taasisi zake na Mfuko wa Bunge kwa mwaka 2025/2026 wakati wa Kikao cha Sita cha Mkutano wa 19 wa Bunge la 12 jijini Dodoma.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge na Uratibu) Mhe. William Lukuvi akitoa ufafanuzi wa baadhi ya Hoja zilizotolewa na Wabunge wakati wa hotuba ya Mhe. Waziri Mkuu kuhusu Mapitio na Mwelekeo wa kazi za Serikali na Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Fedha za Ofisi ya Waziri Mkuu na Bunge kwa Mwaka wa Fedha 2025/2026 wakati wa Kikao cha Sita cha Mkutano wa 19 wa Bunge la 12 Bungeni Dodoma.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Kazi, Vijana, Ajira na Watu Wenye Ulemavu Mhe. Ridhiwani Kikwete akitolea ufafanuzi wa hoja zilizotolewa na baadhi ya Wabunge wakati wa kuchangia Taarifa ya Mapitio ya Utekelezaji wa Kazi za Serikali kwa Mwaka 2024/2025 na Mwelekeo wa Kazi za Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2025/2026. Ofisi ya Waziri Mkuu wakati wa Kikao cha Sita cha Mkutano wa 19 wa Bunge la 12, leo tarehe 5 Aprili, 2025.
Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge na Uratibu) Mhe. Ummy Nderiananga akichangia hoja zilizotolewa na wabunge wakati wa hotuba ya Mhe. Waziri Mkuu kuhusu Mapitio na Mwelekeo wa kazi za Serikali na Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Fedha za Ofisi ya Waziri Mkuu na Bunge kwa Mwaka wa Fedha 2025/2026 wakati wa Kikao cha Sita cha Mkutano wa 19 wa Bunge la 12 Bungeni Dodoma.
Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum Mhe. Dkt. Dorothy Gwajima akiteta jambo na Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge na Uratibu) Mhe. Ummy Nderiananga wakati wa Kikao cha Sita cha Mkutano wa 19 wa Bunge la 12.
Baadhi ya Watendaji wa Ofisi ya Waziri Mkuu pamoja na Taasisi zake wakifuatilia Kikao cha Sita cha Mkutano wa 19 wa Bunge la 12 Jijini Dodoma wakati wa kupitisha bajeti ya Ofisi ya Waziri Mkuu, Taasisi zake na Mfuko wa Bunge kwa mwaka wa fedha 2025/2026.
(PICHA ZOTE NA OFISI YA WAZIRI MKUU)