By ngilishonews.com
MTAALAMU Maarufu wa Tiba asili nchini , kupitia taasisi yake ya Kazoba International Herbal Products amewashauri watoa huduma za tiba asili hapa nchini, kusajili huduma zao pamoja na dawa zao kwa kufuata sheria ili kuunga mkono juhudi za serikali.
Dkt Kazoba mbali na kutoa huduma hiyo ya Tiba asili pia kupitia taasisi yake hiyo amekuwa mdau mkubwa wa kuhamasisha watoa tiba wenzake kusajili dawa zao kwa manufaa yao na wateja wao.
“Katika kuunga mkono juhudi za serikali tunahamasisha watoa huduma wa tiba asili kusajili dawa zao kwani tunanunua dawa za wenzetu zilizosajiliwa na kuzipeleka kwenye maonyesho mbalimbali kama Sabasaba nk ,na hivyo kuwasaidia wahitaji kujua huduma zetu”
“Pia tumefanya ziara katika mikoa ya Dar es Salaam ,ziara iliyohusisha kutembelea mamlaka muhimu kama Mkemia Mkuu wa Serikali, TBS, Botanic, Muhimbili, na Baraza la Tiba Asili na Tiba Mbadala kwa lengo la kupata ushauri juu ya huduma zetu”Alisema Dokta
Alisema Katika ziara hiyo wamekuwa tukirekodi taratibu zinazohitajika ili kupitia mitandao ya kijamii waendelee kuwaelimisha wenzao juu ya umuhimu wa kusajili wa dawa asili .
Pia, tunahamasisha ushiriki wa watoa huduma wa tiba asili katika mafunzo yanayotolewa na vyuo mbalimbali kwa juhudi za Mheshimiwa Rais, Samia Suluhu Hasani huku tukishirikiana na vyombo vya habari kueneza elimu hiyo kwa uwezo wetu wa kifedha.
Katika tafiti zetu, tumekuwa tukitembelea hospitali mbalimbali na kuchunguza magonjwa yanayosumbua jamii na kufanya tafiti dawa zinazoweza kukabiliana na magonjwa hayo.
Tunapoingia kwenye wodi za wagonjwa na kukuta magonjwa 10 tofauti, huwa tunachukua matatu ya mwanzo yanayoathiri watu wengi zaidi na kupeleka changamoto hizo kwa wataalamu wenzetu wa tiba asili vijijini.
Baada ya kupata tiba zinazofanya kazi, tunazipeleka katika mamlaka husika kusajiliwa.
Tunapopata kibali cha DAWA huwa tunawapatia wagonjwa na zinafanyakazi NJ vizuri sana.
Hadi sasa Kazoba International Herbal Products, tunazo dawa zaidi ya 50 kwa magonjwa sugu, ikiwa ni pamoja na:
• UKIMWI (asilimia 95 ya ufanisi na kuendelea
• Shinikizo la damu (kupanda na kushuka)
• Vidonda vya tumbo, hata kwa wanaotapika damu
• Kisukari (Diabetes) tunasaidia ini na kongosho, minyoo na kusafisha (Kuondoa sumu mwilini) na kuiweka sukari sawa.
• Magonjwa ya ngozi, meno, macho, na mengine mengi
Tumefungua vituo vya kuuzia dawa zetu Mwanza, Dar es Salaam, Arusha, na Dodoma.
Pia, tumekuwa tukishirikiana na wasimamizi wa tiba asili katika maeneo haya ikiwemo MARASI, tukiwaalika watoa huduma wengine kujifunza kutoka kwetu kwa namna tunavyo fuata taratibu.
Licha ya watoa huduma wa tiba asili kukumbana na upinzani kwa kuitwa wachawi au matapeli, jambo linaloumiza wengi.
*Kazoba International Herbal Products*, tumeanzisha kiwanda cha tiba asili mkoani Mwanza na kuhudhuria mafunzo ya SIDO, ambapo tumepata vyeti mbalimbali ikiwemo cheti cha heshima kutambuliwa kwa ubora wa huduma tunazotoa.
Pia, tumeomba *TAMISEMI* kutambulishwa kwa makatibu tawala wa mikoa ili tuweze kutoa elimu ya afya na lishe, na tumepokea barua ya pongezi kwa juhudi zetu na ushauri wa kuendelea kushirikiana na mamlaka husika bila kurudi nyuma.
Kwa kifupi,
Tumejitahidi kutafuta suluhisho la changamoto zinazokabili tasnia ya tiba asili.
Changamoto ambazo nyingi husababishwa na tamaa za baadhi ya wahudumu au vita dhidi ya tiba asili.
Kwa kuendelea kujenga utambuzi wa tiba asili kama sekta halali…
Kazoba International Herbal Products tumekuwa mstari wa mbele kusaidia jamii kwa kuchangia katika vituo vya watoto yatima na kusaidiana na serikali yetu.
Tunatambua kuwa afya ni mjumuiko wa mambo mengi, ikiwemo chakula, mavazi,elimu n.k
Tumeweka bei nafuu kwa dawa zetu, na hata kama mgonjwa hana pesa, tunamuhudumia ili kuhakikisha jamii inabaki na nguvu kazi imara.
Tunashirikiana na makundi mbalimbali kama wachimbaji wa dawa, wauzaji, na viwanda ili kuhakikisha tiba asili inakua kwa viwango vinavyotakiwa.
Kutokana na ubunifu wetu, tumeweza kuitangaza tasnia ya tiba asili na kushinda tuzo mbalimbali.
Miongoni mwa mafanikio yetu ni cheti tulichopokea kutoka kwa Naibu Waziri wa Afya kwenye kongamano la Tiba Asili ya Mwafrika lililofanyika Mwanza mwaka 2024.