NAIBU Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Mipango na Uwekezaji Stanslaus Haroon Nyongo (Mb) amesema kuwa Serikali imeendelea kuchukua hatua madhubuti za kuboresha mazingira ya biashara na uwekezaji kwa lengo la kuwawezesha Watanzania na wageni kushiriki kikamilifu katika shughuli za kiuchumi nchini kwa kufanya mapitio ya jumla ya sheria 66 za kisekta.
Nyongo ameyasema hayo leo tarehe 15 Aprili, 2025 wakati wa Kongamano la Kodi na Uwekezaji la mwaka 2025 lenye kauli mbiu (Kuongeza ukuzaji wa rasilimali za ndani kupitia kustawisha fursa za Wananchi) lililofanyika katika ukumbi wa Julius Nyerere (JNICC) Dar ea salaam.
Nyongo ameongeza kuwa mwaka 2019, Serikali ilianzisha na kupitisha Mpango wa Kuboresha Mazingira ya Biashara na Uwekezaji nchini (MKUMBI) kwa lengo la kurahisisha taratibu za udhibiti, kuondoa mwingiliano wa majukumu kati ya taasisi mbalimbali za Serikali, pamoja na kuimarisha matumizi ya TEHAMA katika utoaji huduma kwa wananchi.
Kongamano hilo limefungulia rasmi na Makamu wa Rais, wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. Philip Mpango.