Jaji Mstaafu wa Mahakama Kuu, Dk Fauz Twaib akizungumza wakati wa mafunzo ya kuhusu utatuzi migogoro kwa njia mbadala wa mahakama yaliyoandaliwa na Baraza la Taifa la Ujenzi (NCC) ambayo yamefanyika kwa siku tatu jijini Dar es salaam.
Mkurugenzi Msaidizi kutoka Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali, anayehusika na sehemu ya mikataba, majadiliano na utawala, Mkadiriaji Majenzi Elias Kisamo akijibu maswali tatizi yaliyoulizwa na washiriki wa mafunzo utatuzi migogoro kwa njia mbadala wa mahakama yaliyoandaliwa na Baraza la Taifa la Ujenzi (NCC) ambayo yamefanyika kwa siku tatu jijini Dar es salaam.
Mhandisi wa kujitegemea, Julius Mamiro akifundisha washiriki wa mafunzo mbinu ya utatuzi migogoro kwa njia mbadala wa mahakama ambayo yaliyoandaliwa na Baraza la Taifa la Ujenzi (NCC) ambayo yamefanyika kwa siku tatu jijini Dar es salaam.
Baadhi ya washiriki wa wa mafunzo ya kuhusu utatuzi migogoro kwa njia mbadala wa mahakama yaliyoandaliwa na Baraza la Taifa la Ujenzi (NCC) ambayo yamefanyika kwa siku tatu jijini Dar es salaam.
Picha ya pamoja wakufunzi na washiriki wa wa mafunzo ya kuhusu utatuzi migogoro kwa njia mbadala wa mahakama yaliyoandaliwa na Baraza la Taifa la Ujenzi (NCC) ambayo yamefanyika kwa siku tatu jijini Dar es salaam.
……………………
-Yaelimisha namna ya kuitatua bila kujeruhi upande wowote
Na Mwandishi wetu
BARAZA la Taifa la Ujenzi (NCC) limesema uwezekano wa migogoro ya kibiashara, madai ya kimkataba na mingine iliyopo na inayojitokeza kwenye sekta mbalimbali nchini, ikiwemo ya ujenzi, inawezekana bila wahusika wa migogoro hiyo kupelekana mahakamani.
Hali hiyo, kwa mujibu wa wataalamu wa masuala hayo ya usuluhishi na utatuzi wa migogoro wanaotoa mafunzo kuhusu eneo hilo, chini ya uratibu wa NCC, inasaidia si tu kuokoa muda na kuacha wahusika wakiwa na amani, bali inapunguza mirundikano ya kesi mahakamani.
Akizingumza Dar es Salaam hivi karibuni wakati mafunzo hayo yaliyoandaliwa na NCC yakiendelea, Jaji Mstaafu wa Mahakama Kuu, Dk Fauz Twaib ambaye ni miongoni mwa wafundisha njia hizo, alisema: “Kinachotakiwa ni wasuluhishi kuzingatia maadili, sheria na taratibu za usuluhishi”.
Alisema njia zaidi ya nne za kusuluhisha migogoro mbali na kushitakiana mahakamani, zinafundishwa na kuwawezesha waliopata mafunzo hayo kuamua kwa weledi ipi inafaa kulingana na mazingira na hali halisi ya mgogoro husika.
Kwa mujibu wa Dk Twaib, Kwa kutumia njia hizo mbadala, hakuna upande unaojeruhiwa, kwa sababu pande zote zinahusika katika hatua zote muhimu za usuluhishi, ikiwemo kuchagua nani ahusike kuwasuluhisha.
“Ikiwa hakuna mazingira yoyote ya tamaa inayoweza kusababisha upendeleo, mfano rushwa au chochote kile kitakachofanya usuluhishi uegemee upande mmoja, mlolongo wa kisuluhishi hautokei, hivyo kuokoa muda na gharama.
Kwa upande wake, Mhandisi wa kujitegemea, Julius Mamiro anayefundisha mbinu hizo, hususan majadiliano ya kisuluhishi ya madai ya kimkataba ya ujenzi alisema, maadili mazuri yanafanikisha usuluhishi.
Alisema, jambo kubwa wanalolisisitiza ni wataalamu wa masuala yote yanayoweza kuhusika kwenye migogoro, iwe ya sekta ya ujenzi au ya kibiashara nje ya sekta ya ujenzi au ya kimkataba kwenye sekta yoyote, wawe na elimu ya namna ya kuitatua migogoro yao bila kupelekana mahakamani, kisha watekeleze mbinu walizofundishwa kwa kuzingatia maadili.
Kwa maelezo yake, kujua kusuluhisha au kutatua mgogoro halafu ukauharibu utatuzi kwa kutoruhusu haki au kwa kupendelea, hata kama umefunzwa vipi, unabaki kuwa kikwazo cha usuluhishi.
“NCC inatekeleza jukumu la kuhakikisha elimu hiyo inawafikia watu wengi, kwa faida ya wanaoipata, wateja wao, familia zao na Taifa kwa ujumla.
Alisema, kutokana na umuhimu huo, anawashauri Watanzania kuchangamkia mafunzo hayo pindi wanaoipata fursa hiyo nyakati zote yanapotangazwa.
Katika mafunzo hayo yaliyotolewa kwa siku tatu, washiriki walifanya mazoezi ya usuluhishi kwa vitendo na kisha kutahiniwa kwa mtihani wa kuandika, lengo likiwa kupima uelewa wao kuhusu maarifa waliyapata kwenye mafunzo hayo.
Mkurugenzi Msaidizi kutoka Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali, anayehusika na sehemu ya mikataba, majadiliano na utawala, Mkadiriaji Majenzi Elias Kisamo, pamoja na kufundisha, alijibu maswali tatizi yaliyoulizwa na washiriki wa mafunzo hayo, hivyo kuongeza uelewa wao juu ya walichojifunza.
Kisamo alisema,” Ukitaka usuluhishi uende sawa, epuka njia za mkato. Hakuna shortcuts, iwe katika majadiliano au kwenye utatuzi mwingine, epuka ‘shortcuts’…