https://p.dw.com/p/4hd1X
Biashara na maduka yamefunguliwa huku wananchi wakiripotiwa kuendelea na shughuli zao za kawaida.
Maandamano yaliyoongozwa na vijana yalizuka wiki hii baada ya bunge la kitaifa kuupitisha mswada tata wa fedha uliotoa mapendekezo ya kuongeza ushuru kwa mkate na mafuta ya kupikia.
Soma pia:Mahakama Kenya yaidhinisha kutumiwa jeshi kutuliza ghasia
Rais wa Kenya William Ruto alisema hatoutia saini mswada huo wa fedha kufuatia shinikizo la umma.