Waziri mkuu Kassim Majaliwa mgeni rasmi Great Ruaha Marathon

Mkuu wa Mkoa wa Iringa Peter Serukamba amewakaribisha wakazi wa mkoa huo kujitokeza kushiriki Mbio za Great Ruaha Marathon ili kuendelea kuupa thamani Mkoa katika utalii.

Serukamba amezungumza hayo leo akiwa ofisini kwake ambapo huku akitaja kuwa Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Kassim Majaliwa ndiye anayetarajiwa kuwa Mgeni rasmi katika msimu huu wa mbio hizo.

Mbio hizo zitafanyika Julai mosi 2024 katika hifadhi ya Wanyama pori ya Ruaha inayopatikana mkoani Iringa huku lengo kuu likiwa ni kuendelea kukuza utalii wa ndani kama anavyosisitiza Rais Samia Suluhu Hassan.

“Ninawakaribisha wanairinga wote kushiriki mbio hizi za Great Ruaha Marathon kwa sababu mazoezi ni afya na kubwa zaidi tunautangaza Mkoa wetu katika sekta ya utalii”, amesema Serukamba.

Mpaka sasa zaidi ya watu 400 wamejiandikisha kushiriki mbio hizo kwa mwaka huu huku wakitarajiwa kuwa idadi kubwa zaidi ya msimu uliopita.

Related Posts