MABINTI WENGI WANA VIDONDA VYA OPERATION HII NI HATARI – AFISA NJOMBE

Mratibu wa mama na mtoto mkoa wa Njombe Felisia Hyera ametoa wito kwa wazazi na walezi kutunza vizuri familia zao ikiwemo pia kuimarisha lishe ya familia pamoja na kusimamia makuzi ya watoto ili kuepusha mimba za utotoni ambazo pia zimekuwa zikisababisha mabinti wengi kuingia kwenye upasuaji hali inayopelekea kuwa na kizazi chenye ulemavu kwa kushindwa kufanya kazi.

Ametoa wito huo kwenye kikao cha utekelezaji wa programu Jumuishi ya Taifa ya Malezi,Makuzi na Maendeleo ya awali ya mtoto (PJT-MMMAM) unaotekelezwa na shirika lisilo la kiserikali la UWODO kwa kushirikiana na serikali ambapo amesema kitendo cha wanawake wengi kufanyiwa upasuaji ni hatari kubwa kwa kuwa taifa linazalisha walemavu kwa kushindwa kufanya kazi.

“Tunakutana na mabinti wengi wenye vidonda vya upasuaji na hii ni hatari kwasababu tukifanya upasuaji leo ujue ujauzito utakaofuata pia ni upasuaji kwa hiyo tunatengeneza vilema huko mtaani unakutana na binti mdogo anasema baridi inanisumbua ujue huyo shambani haendi na huwezi ukampa heka heka,hapo tunaharibu kizazi chetu kwa kuwa na vilema ambao hawafanyi kazi kama tunavyotarajia”amesema Felisia Hyera

Naye mkurugenzi wa shirika la UWODO bwana Hamis Kassapa ametoa wito kwa wazazi kuhakikisha watoto wanakuwa katika malezi,makuzi na tamaduni zetu ili kuondokana na adha mbalimbali ikiwemo ya kuua watoto pamoja na udumavu unaoendelea kutesa jamii hususani watu wa mkoa wa Njombe.

Related Posts