Viongozi wa Chama cha ACT Wazalendo jimbo la Kilindi mkoani Tanga jana tarehe 30 Juni 2024 wamehamia Chama cha Demokrasia na Maendeleo Chadema. Anaripoti Faki Ubwa … (endelea).
Viongozi hao wamepokewa na Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika Kilindi mkoani humo.
Viongozi wa ACT waliohamia Chadema ni pamoja na:-Salum Omar – Mwenyekiti wa Jimbo, Mhina Magoma – Katibu wa Jimbo, Siwema Hassan – Afisa Mipango na Uchaguzi, Mwajabu Khatibu – Mwenyekiti Ngome ya Wanawake Jimbo, Mohamed Hamisi – Katibu Ngome ya Wazee Jimbo na Lazaro Leonard – Katibu wa Kata tya Kwidibom.